Na Mwandishi wetu, Mirerani

CRDB Benki Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kukutana na wateja wao kupitia kauli mbiu ya 'mission possible'.

Meneja wa CRDB Tawi la Mirerani, Renatus Rutajama akizungumza na wateja hao wakati wakipata kifungua kinywa pamoja amesema benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao.

Rutajama amesema katika kuhakikisha benki hiyo inawafikia wananchi wengi zaidi, imejipanga vyema kutokana na maboresho ya mifumo kidigitali akieleza kuwa walimu, wanafunzi, watumishi wa umma na sekta binafsi wamefikiwa wote.

Amesema hali hiyo ni kutokana na kuaminiwa na wateja wao kufuatia huduma zao kukubalika na wameboresha mifumo ambapo mwanafunzi, mwalimu na mtu yeyote anaweza kupata huduma popote kupitia simu yake.

Amesema wiki ya huduma kwa mteja inaenda sambamba na miaka 30 ya kuwapo kwa benki hiyo ambayo ina matawi hadi nje ya nchi ikiwemo Congo DRC na Burundi.

Nipende kuwashukuru wateja wetu kwa kuchukua muda wao na kuja kutuunga mkono bila kuwasahau wafanyakazi wenzangu wa CRDB kwa namna tunavyofanya kazi," amesema Rutajama.

Afisa mwingine wa benki ya CRDB Tawi la Mirerani, Adam Mgaza amesema ikiwa ni wiki ya pili ya kila mwezi wa 10 huwa wanafanya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Mgaza ameeleza kwamba wanatarajia kupiga hatua kubwa zaidi kwa upande wa kutoa huduma kwa wateja wao kulipia kauli mbiu ya 'Mission Possible'.

Mmoja kati ya wateja wa benki hiyo, Peris Mwanyika ameipongeza CRDB kwa kuboresha huduma kwa mawakala wao kwani hivi sasa wanaweza kuwapatia wateja wao hadi shilingi milioni 30.

Hata hivyo, Peris amepongeza hatua hiyo na kuwasihi viongozi hao wafanikishe hadi wateja wao waweze kutoa shilingi milioni 50 kwa mawakala.

Mwenyekiti wa mtaa wa Manyara, Rogathe Kweka amesema CRDB ni miongoni mwa taasisi za fedha zinazosababisha jamii kupiga hatua kimaendeleo.

Kweka amesema ameona wajasiriamali wengi wanaonufaika na huduma za mikopo kupitia CRDB na wakaondokana na mikopo isiyo rafiki ya kausha damu.

Sheikhe wa baraza kuu la waislamu Tanzania (Bakwata) wilaya ya Simanjiro, Ramia Isanga ameipongeza CRDB kwa kuwa baraka kwao kwa kutoa huduma ya akaunti ya Albaraka ambayo haina riba.

Sheikhe Isanga amesema akaunti hiyo haina riba ina faida jambo ambalo ni maneno mawili ambayo yana maana tofauti.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...