Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Serengeti

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Wanawake wanauwezo mkubwa wa kuongoza taifa katika nafasi mbalimbali tofauti na baadhi ya watu wanaodhani kwamba wanaoweza ni wanaume peke yao.

Dk.Samia ameyasema hayo leo Oktoba 10,2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara alipokuwa akiendelea na mkutano wa kampeni kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.

“ Pamoja na mila na desturi zenu suala la umoja na mshikamano wa Watanzania ni suala muhimu sana.Vilevile  Mungu alivyotuumba hakuumba kwamba mwenye kichwa fulani alichozaliwa nacho kwamba anaakili kuliko mwenzake.”

“Pia hatukuambiwa kwamba mwanamke ana akili zaidi kuliko mwanaume au mwanaume ana akili zaidi kuliko mwanamke.Mwenyezi Mungu alitutofautisha kwenye zile kazi ambazo alizotupa kazi ambazo alituambia wanawake tutabeba ujauzito na kuzaa kwa uchungu na akatuumba kwa maumbile hayo.”

Akieleza zaidi Dk.Samia amesema wanaume waliambiwa wao ni wasimamizi wa wanawake na watakuwa na kazi ya kutunza familia zao. “Lakini jinsi tunavyokwenda wanawake wanafanyakazi na kutunza familia zao.

“Nasema hivi kwa sababu nimeanza kusikia maneno kwamba mgombea wetu huyu ni mwanamke na kwa mila na desturi zetu hatutaki mgombea mwanamke.”

Amefafanua kuwa katika maendeleo hakuna mwanamke hakuna mwanamke na kwamba yeye aliyesimamq mbele yao ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya miaka minne amefanyakazi kubwa.

“Ingekuwa mwanamke hawezi nisingeweza kuyafanya yote niliyofanya. Mungu ametuumba wote kwa akili sawa, uwezo wa kufikiri, ukiwa mwanaume unafikiri ukiwa mwanamke unafikiri.Tena mwanamke ni mwaminifu zaidi na mtendaji zaidi kwa sababu ya uoga kuliko mwanaume.”

Mgombea Urais Dk.Samia amesisitiza pamoja na mila na desturi zilizopo nchini ameqnza kusikia maneno kwamba CCM mkoani Mara wanasema wamepewa wagombea wanawake.”Kwani wanawake wana nini?.”

“Nataka niwaambie wanawake wanachapakazi kama wengine wanavyochapakazi. Mkoa huu utaendelezwa na wanawake na wanaume kwa mshikamano.Tanzania hii itaendeshwa na kuendelezwa mambo yake na wanaume na wanawake wote kwa umoja wetu. Cha muhimu hapa sote ni watanzania, sote ni wataifa moja.”

“Tushikamane tuijenge nchi yetu kama waasisi wetu walivyotuambia. Yale ya huyu mwanamke huyu mwanaume hayapo.Ulimwengu unajengwa na wanawake na wanaume, kuna wanasayansi wanawake na wanaume.

“Kuna madaktari wanawake na wanaume na unapokwenda hospitali husemi huyo daktari mwanamke asinitubu. Unatibiwa na mwanamke na mwanaume.Unapolindwa na askari wetu unalindwa na wanawake na wanaume au tumesema askari wetu wanawake hawafai kulinda? Wanapangwa malindo na Tanzania yetu ipo salama.”

Ameeleza zaidi Dk.Samia ameeleza kwamba hata yeye alipoingia madarakani kuna waliobeza kwamba sitoweza.”Leo tunazungumza mengine.”









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...