Na Victor Masangu,Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, amekabidhi rasmi magari sita kati ya 11, boti moja kubwa magari mawili ya wagonjwa mawili kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Mkoa huo yenye thamani ya Sh. bilioni 7.9.
Kunenge,amekabidhi vifaa hivyo kwa Kamanda wa kik cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Pwani Jenifa Shirima katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Pwani iliyopo Manispaa ya Kibaha.
Hafla hiyo imehudhuriwa na watendaji wengine mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema, Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani pamoja na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Mkoa huo.
Awali,akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo Kunenge ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha vitendea kazi vya vyombo vya ulinzi na usalama hususani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Amesema upatikanaji wa magari na boti hizo utaimarisha uwezo wa Jeshi hilo katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuokoa maisha na mali za wananchi wakati wa majanga ya moto na maafa ya majini.
“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika vifaa vya uokoaji na uboreshaji huu utasaidia kuongeza ufanisi katika kazi za zimamoto na kuimarisha usalama wa wananchi wetu", amesema Kunenge.
Aidha, Kunenge amelipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Mkoa wa Pwani kwa kazi nzuri ya kupambana na matukio ya moto na majanga mbalimbali ambapo amesema upatikanaji wa vifaa itawaongezea ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani, Jenifa Shirima, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulipa jeshi hilo kipaumbele katika upatikanaji wa rasilimali na vifaa muhimu.
Amesema magari na boti vilivyokabidhiwa vitasaidia kwa kiasi kikubwa katika majukumu ya uokoaji, ikiwemo usafirishaji wa wagonjwa, kudhibiti moto, na kutoa huduma za haraka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani.
“Vifaa hivi vitasaidia kuongeza kasi ya majibu wakati wa dharura na kupunguza madhara yanayosababishwa na majanga ya moto na ajali hivyo tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa kuboresha huduma za zimamoto nchini,” amesema Kamanda Shirima.
Hatahivyo makabidhiano hayo ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuhakikisha taasisi za ulinzi na usalama zinakuwa na vifaa vya kisasa vinavyowezesha utoaji wa, wa huduma bora kwa wananchi.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...