Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
WASHIRIKI kutoka nchini 16 ikiwemo Tanzania wameshiriki Kongamano la Tano la Uongozi Wanawake lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi(Uongozi Institute)chini ya dhima ya Mchango wa wanawake katika uongozi barani Afrika.
Kongamano hilo leo Oktoba 6,2025 jijini Dar es Salaam na miongoni mwa nchi ambazo zimeshiriki ni Kenya, Afrika ya Kusini, Rwanda, Gambia, Zambia, Nigeria, Liberia na mwenyeji Tanzania.
Akizungumza katika ufunguzi wa Jukwaa hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi,Kadari Singo amesema washiriki hao ambao ni wanawake wamekutana kwaajili ya Jukwaa la Uongozi wa maendeleo endelevu lengo likiwa ni kuendeleza wanawake katika suala la Uongozi kwa Afrika.
“Lengo la Taasisi ya Uongozi ni kuwafikia wanawake viongozi barani Afrika katika kuhakikisha wanajengewa uwezo ili wanapochukua nafasi za uongozi waweze kutumikia vema. Takwimu zinaonesha mpaka sasa kuna asilimia 33 pekee yake wanaoshikilia nafasi kubwa za maamuzi duniani.
“Kwa kasi hii inaonesha kuwa itachukua miaka 130 kufikia 50 kwa 50 kama spidi itakuwa haijaongezeka.Taasisi ya Uongozi imeendelea kufanya jitihada kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwajengea uwezo wanawake wengi zaidi wenyesifa kushika nafasi ya uongozi.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt.John Jingu alipokuwa akizungumza wakati akifungua kongamano hilo amesema kuzinduliwa kwa programu hiyo kutasaidia washiriki wa kongamano hilo kujengewa uwezo.
''Washiriki waliopo katika mafunzo haya nimeambiwa kuwa mnakuwa na walezi wenu katika maeneo mbalimbali,kama kwenye biashara au Serikalini,ili wawajengea uwezo sehemu ambazo mpo.”
Akieleza zaidi amesema kupitia kongomano hilo ni kwmba wanatengenezwa waleta mabadiliko,katika jamii yetu ya Bara la Afrika katika shughuli za maendeleo na hivyo kuwa na mafanikio.
Wakati huo huo Balozi wa Finland nchini Tanzania,Theresa Zitting wakati anazungumza ameeleza uongozi sio kuhusu nafasi bali ni kuhusu wao wenyewe kuvumilia na kutoshindwa hivyo ni vema wanawake hao wasiogope kuanguka bali wasimame na kujaribu.
Hata hivyo wakati wa jukwaa hilo imeelezwa ufunguzi wa Jukwaa hilo linafanyika kama sehemu ya Programu ya Uongozi kwa Wanawake (Women’s Leadership Programme) ya Taasisi ya UONGOZI, yenye lengo la kukuza nafasi za uongozi kwa wanawake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...