Na Mwandishi wa OMH
Kibaha, Pwani. Serikali imeeleza dhamira yake ya kutengeneza sheria rafiki za uwekezaji zitakazoiwezesha kufikia uchumi wa kati wa juu kama ilivyobainishwa kwenye Dira 2050.
Moja ya shabaha za Dira 2050 ni kuchochea ukuaji wa Pato la Taifa kutoka zaidi ya $80 billioni za sasa mpaka $1 trilioni ifikapo mwaka 2050.
Kufikia lengo hilo, serikali imesema ni lazima iendelea kutengeneza mazingira mazuri ya biashara yatakayowezesha taasisi za umma kufanya vizuri kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Hayo yalisemwa Alhamisi, Oktoba 16, 2025 wakati wa kikao kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria, kilichofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu alisema maagizo waliyopewa na Mhe. Rais. Dk. Samia Suluhu Hassan, ni uboreshwaji wa sheria ili ziendane na maono yaliyomo kwenye Dira 2050.
“Tunapaswa kuwa na sheria ambazo zitaongeza ufanisi wa taasisi za umma. Tunapaswa kuwa na sheria ambazo zitatoa wigo kwa sekta za umma kufanya kazi kwa ukaribu na sekta binafsi,” alisema Bw. Mchechu.
Alisema kuongezeka kwa ufanisi wa sekta za umma, kutapelekea ongezo la mchango wake kwenye mapato ya ndani ya serikali kutoka asilimia nne ya sasa mpaka kufikia kumi miaka minne ijayo, kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais Samia.
“Tunapaswa kuboresha huduma na bidhaa zetu, pamoja na kupunguza matumizi yasiuyokuwa ya lazima, ili kuongeza mapato na hatimaye gawio kwa serikali,” alisisitiza Bw. Mchechu.
Serikali inataka kuona tija katika uwekezaji wake wa Sh92.3 trilioni ilioufanya katika taasisi za umma na kampuni ambazo ina umiliki wa hisa chache.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno alisema kuwa uimara wa taasisi za umma na sekta binafasi unategemea ubora wa sheria zinazosimamia uwekezaji.
Alieleza kuwa usimamizi wa mikataba ya uwekezaji usipokuwa mzuri, itakuwa ngumu au itachukua muda mrefu kufikia matarajio yaliyowekwa na serikali.
“Aidha, hali hii inaweza kuibua migogoro na hivyo kupelekea kuwakatisha tamaa wawekezaji,” alisema huku akibainisha kuwa serikali haiko tayari kufikia hatua hiyo.
“Eneo hili la usimamizi wa mikataba tunalipa kipaumbele kikubwa. Kwa mwaka mmoja wa fedha tunaweza kusimamia kati ya mitaba 15,000 na 20,000.
“Na ili kufanya usimamizi wa mikataba hii uwe wa ufanisi, tumeona haja ya kukumbatia matumizi ya teknolojia ili kurahisisha ufuatiliaji.”
Aidha, alielezea haja ya kuepuka urasimu usiokuwa wa lazima ili wawekezaji, hasa katika eneo la ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Dk. Ally Possi, alisema sheria za nchi hazitakiwa ziwe kikwazo kwa wawekezaji, badala yake kivutio.
“Ili ndoto yetu ya kuwa na uchumi unaofikia $1 trilioni, ifikie, tunapaswa kuendelea kutengeneza mazingira rafiki ya biashara yatakayovutia wawekezaji zaidi,” alisema.
Sanjari na hilo, Dk. Possi alisema nchi inapaswa kuendelea kuboresha usimamizi wa mikataba, hususani katika eneo la PPP.
Aidha, alisema taasisi za umma zina jukumu la kutoa gawio na kukuza Uchumi wa nchi.
“Lakini hili haliwezi kutimia ikiwa taasisi hizo zitagubikwa na kesi ambazo zitazilazimu kulipa fedha baada ya hukumu ya mahakama kutolewa, na ni katika muktadha huo tumekutana kujadili namna bora ya kukabiliana na mapungufu ya kisheria,” alihitimisha Dk. Possi.
Naye Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole alisema kufikia Uchumi wa $1 trilioni unategemea uimara wa taasisi za umma na ndio maana ipo haja ya kuwa na mfumo imara wa kisheria katika eneo la uwekezaji.
“Ni lazima mashirika ya umma yasimamiwe na sheria za uwekezaji ambazo zinaendana na mahitaji ya sasa,” alisema.
“Mfumo wa sheria lazima uendane na kasi ya ukuaji wa uwekezaji katika mashirika ya umma.”

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akizungumza katika kikao kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria, kilichofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...