NA Mwandishi wetu
MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na dhamana Tanzania (CMSA) imeeleza kuwa mfuko wa pamoja wa uwekezaji Vertex International Securities Exchange Traded Fund (Vertex ETF)” ni wa kuigwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama, ameyasema hayo leo wakati wa tukio la kihistoria katika Soko la Hisa La Dar es Salaam (DSE) baada ya kuorodheshwa kwa mfuko huo kwenye soko hilo.

Amesema mafanikio hayo makubwa ni kutokana na mamlaka ya masoko (CMSA) kushusha kiwango cha ushiriki kutoka sh 1,000,000 hadi sh 20,000 ambapo imewezesha wawekezaji wengi mmoja mmoja kuweza kushiriki.
"Siku muhimu ya kihistoria katika soko la mitaji, mfuko wa kwanza kuuza hisa ya vipande kuorodheshwa katika soko la hisa jambo jema ambalo linawapa nafasi kubwa wawekezaji kuwekeza, na pia tunazitaka kampuni nyingine kuiga mfano wa Vertex kuja na bidhaa bunifu kama hizi,"amesema Mkama.
"Ni furaha kubwa kujumuika nanyi leo hii kushuhudia tukio hili la kihistoria ambalo lina mchango mkubwa katika maendeleo na ustawi wa masoko ya mitaji na uchumi kwa ujumla hapa nchini,"
.jpeg)
Aidha Mkama amesema kwa namna watu walivyoudhuria ni uthibitisho kwamba sekta ya masoko ya mitaji nchini ina wadau wengi wanaounga mkono utekelezaji wa mikakati inayosimamiwa na (CMSA) ya kuanzisha bidhaa mpya na bunifu zinazotoa wigo mpana kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kushiriki katika uwekezaji kwenye masoko ya mitaji hapa nchini.
"Mfuko wa Vertex ETF una tofauti na mifuko mingine ya uwekezaji wa pamoja iliyoidhinishwa na CMSA, kwani Mfuko huo unaorodheshwa kwenye soko la hisa; na kutoa fursa kwa wawekezaji kuuza na kununua vipande vya mfuko ambao unawekeza kwenye kampuni zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa.
Mkama amesema "mfuko huu umebuniwa kimkakati kwa lengo mahsusi la kuwekeza kwenye kampuni zenye utendaji mzuri zaidi, na hivyo kuongeza ukwasi katika soko la hisa na kupanua ushiriki wa wawekezaji katika masoko ya mitaji.

Amesema Mfuko wa Vertex ETF utawekeza kwenye hisa za kampuni zilizoorodheshwa Soko la Hisa la Dar es Salaam, ambazo zina utendaji mzuri zaidi.
"Uwekezaji utaanza kwenye hisa za Benki ya CRDB, Benki ya NMB, Kampuni ya Uwekezaji ya NICO - National Investment Company Limited (NICO), Dar es Salaam Stock Exchange PLC (DSE) na Kampuni ya AFRIPRISE. Lengo la uwekezaji wa aina hii ni kuufanya mfuko huu kuwa na ukwasi wa kutosha kukidhi mahitaji ya fedha kwa wawekezaji pindi yanapotokea".
Amesema (CMSA) ina jukumu la kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba shughuli katika masoko ya mitaji zinafanyika kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili kuleta uwazi na haki kwa washiriki wote.
.jpeg)
"Kama tulivyoshuhudia mauzo ya vipande vya mfuko wa Vertex ETF yamepata mafanikio ya asilimia 136, ambapo kiasi cha sh billioni 6.8 kimepatikana, ikilinganishwa na lengo la sh.bilioni 5.
Aidha, asilimia 82.2 ya mauzo ya vipande imetoka kwa wawekezaji mmoja mmoja na asilimia 17.8 imetoka kwa Kampuni na taasisi.
Naye Mtendaji Mkuu wa Vertex International Securities, Mateja Mgeta, amesema wakati wanaanza kuuza vipande hivyo lengo ilikuwa kupata bilioni tano kwani kipande kimoja cha mfuko kilikuwa kinauzwa sh. 200, hadi zoezi la mauzo ya awali linakamilika waliweza kupata bilioni 6.8 Sawa na asilimia 136 na kuvuka lengo
Mgeta amesema mfuko wa ETF umeweza kupata idadi ya wawekezaji zaidi ya 6,300 na katika hao kuna wawekezaji wapya hali inayoenda sambambamba na Serikali katika masuala ya uchumi jumuishi.
.jpeg)
"Vertex inapenda kutoa ahadi kwa Watanzania na wawekezaji wote kwa ujumla kwamba itasimamia huu mfuko kwa weledi ili kuhakikisha wawekezaji wanafaidika na matunda ya uwekezaji wao na kuendelea kuleta bidhaa bunifu sokoni zitakazokidhi mahitaji ya masoko ya mitaji na dhamana nchini.
Mgeta amesema ETF imevuka lengo na kuanzia sasa itapatikana katika soko la hisa.
Mecklaud Edson, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Peter Nalitolela amesema zaidi ya miaka 20 toka kuanzishwa kwa soka la hisa hawakuwahi kuwa na bidhaa kama hii ya Vertex.
"Tunawasihi Watanzania waje soko la hisla Dar es Salaam wataipata bidhaa hii nzuri kabisa ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa,".

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...