NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHULE ya Sekondari Bethsaida, inayolea na kusomesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu, imewaomba Watanzania na wadau wa maendeleo kujitokeza kufadhili taasisi hiyo ili kuiwezesha kuendelea kutoa huduma bora ya malezi, elimu na malazi kwa watoto wanaowahudumia.
Ombi hilo limetolewa Oktoba 18, 2025 jijini Dar es Salaam katika mahafali ya Kidato cha Nne ya shule hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa Bethsaida, Bw. Raymond Machary, aliyeeleza kuwa tangu mlipuko wa UVIKO-19 na kuzuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine, ufadhili kutoka ndani na nje ya nchi umepungua kwa kiwango kikubwa.
“Kupungua kwa wafadhili kumeathiri uendeshaji wetu. Tuna mpango wa kupanua majengo ili tuongeze udahili wa watoto wenye uhitaji, lakini tumeelemewa kifedha,” alisema Machary.
Amefafanua kuwa malengo ya taasisi hiyo ni kuhakikisha pamoja na masomo ya kawaida, watoto wanaohitimu wanapata pia ujasiriamali na elimu ya ufundi ili waweze kujitegemea baada ya shule.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule, Bw. Erasto Emmanuel, amesema kupungua kwa ufadhili kumesababisha kupungua kwa idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa ili taasisi iendelee kuhimili gharama za huduma walizonazo kwa sasa.
“Tunawakaribisha wadau kufadhili mwanafunzi mmoja mmoja kwa kugharamia chakula, mahitaji ya msingi au mishahara ya walimu. Tukipata nguvu hii, shule itaendeshwa bila kuyumba,” alisema.
Amesema ukosefu wa wafadhili wa kudumu pia umesababisha baadhi ya watumishi kuondoka kutokana na changamoto za kifedha, hali inayodhoofisha utendaji wa taasisi hiyo.
Katika mahafali hayo, mwanafunzi Alfavarist Kivuyo alitaja changamoto walizonazo kuwa ni upungufu wa maji safi, uhaba wa vitabu vya masomo ya sayansi pamoja na chakula kwa wanafunzi.
Naye mzazi Bi. Diana Benjamin ameishukuru Bethsaida kwa malezi na fursa inayowapatia watoto, huku akiwataka wazazi na jamii kushirikiana na shule hiyo ili kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu badala ya kuwatelekeza.
Shule ya Bethsaida ilianza kwa kuwalea watoto 29, na hadi mwaka 2025 tayari imefadhili wanafunzi 109 kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Nne.

Aidha amesema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma ambapo wanafunzi wengi wanaomaliza wamekuwa wakichaguliwa kuendelea na masomo katika shule mbalimbali za sekondari nchini.
“Mwaka jana wanafunzi wote waliweza kuendelea na masomo, tulikuwa na idadi kubwa ya waliopata Division One na Two, huku waliopata Division Three wakiwa saba tu,” amesema Bw. Machary.
“Mwaka jana wanafunzi wote waliweza kuendelea na masomo, tulikuwa na idadi kubwa ya waliopata Division One na Two, huku waliopata Division Three wakiwa saba tu,” amesema Bw. Machary.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule, Bw. Erasto Emmanuel, amesema kupungua kwa ufadhili kumesababisha kupungua kwa idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa ili taasisi iendelee kuhimili gharama za huduma walizonazo kwa sasa.
“Tunawakaribisha wadau kufadhili mwanafunzi mmoja mmoja kwa kugharamia chakula, mahitaji ya msingi au mishahara ya walimu. Tukipata nguvu hii, shule itaendeshwa bila kuyumba,” alisema.
Amesema ukosefu wa wafadhili wa kudumu pia umesababisha baadhi ya watumishi kuondoka kutokana na changamoto za kifedha, hali inayodhoofisha utendaji wa taasisi hiyo.
Katika mahafali hayo, mwanafunzi Alfavarist Kivuyo alitaja changamoto walizonazo kuwa ni upungufu wa maji safi, uhaba wa vitabu vya masomo ya sayansi pamoja na chakula kwa wanafunzi.
“Tunaiomba serikali na wafadhili watusaidie pia kupata fursa za kufanya ‘tour’ za kielimu katika maeneo mbalimbali ili kuongeza uelewa wetu,” amesema Kivuyo.
Naye mzazi Bi. Diana Benjamin ameishukuru Bethsaida kwa malezi na fursa inayowapatia watoto, huku akiwataka wazazi na jamii kushirikiana na shule hiyo ili kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu badala ya kuwatelekeza.
Shule ya Bethsaida ilianza kwa kuwalea watoto 29, na hadi mwaka 2025 tayari imefadhili wanafunzi 109 kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Nne.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...