Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, kampuni ya Smartpika kupitia Mradi wa Huduma za Kisasa za Upikaji (MECS) imegawa majiko sanifu ya umeme katika Shule ya Msingi Kibasila jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufikia nyumba milioni tano nchini.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Smartpika, Andron Mendes, alisema mpango huo unalenga kuwafikia Watanzania milioni 20 ifikapo mwaka 2034, kwa lengo la kuwawezesha kutumia nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano na Ushirikiano wa Smartpika, Bobu Yona, alisema kampuni hiyo imejipanga kusaidia kupunguza gharama za matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia teknolojia rahisi na rafiki kwa mazingira.
Naye Mwakilishi wa Mradi wa MECS, Charles Barnabas, alibainisha kuwa matumizi ya majiko sanifu ya umeme ni nafuu zaidi na yanachangia kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa.
Akitoa shukrani kwa niaba ya shule, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kibasila, Halima Hassan, alisema majiko hayo yamepunguza gharama za mapishi shuleni pamoja na kulinda afya za wapishi kutokana na kupungua kwa moshi wa nishati chafu.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...