Mwandishi Wetu, Dodoma.
Tanzania kwa nafasi yake ya Uenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (AGN) itaongoza na kubeba sauti ya pamoja ya vipaumbele vya Bara la Afrika wakati wa Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP30).
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema hayo JijiniDodoma Oktoba 21,2025 wakati akifungua Kikao cha Makatibu Wakuu cha maandalizi ya COP 30 utakaofanyika Brazil kuanzia Novemba 10 hadi 21, 2025.
Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,alizindua Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 (Dira 2050) Julai 17, 2025, akiithibitisha nia ya Serikali ya kuwa na maendeleo yenye ustahimilivu wa mabadiliko ya tabiahchi na kuwa taifa lenye ustawi, jumuishi na endelevu, ambapo kila sekta ya maendeleo Nchini inatakiwa kuzingatia dhana ya maendeleo endelevu.
“Mwaka huu COP30 ni ya kihistoria kwa kuwa mkutano huu utafanyika katika nchi yenye historia ya kuanzishwa kwa Mkataba husika na hivyo ajenda zitakazojadiliwa zinatarajiwa kufafanua njia na hatua za haraka hususan katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi baada ya miaka 33 ya uwepo wa Mkataba.
“Kwa Tanzania, Mkutano huu sio wa majadiliano tu bali utahusika pia katika kuongeza mashirikiano na wadau mbalimbali duniani kwa lengo la kuongeza fedha za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zitachangia katika kukuza uchumi na kuimarisha maendeleo ya Kijani Nchini.” Amesema Luhemeja.
Ameongeza katika kuhakikisha hili, Serikali imeanza kuandaa nyezo za utekelezaji vipaumbele vya Dira, na kwa sasa, Serikali ipo katika mchakato wa kukamilisha mipango miwili muhimu ambayo ni Mchango wa tatu wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchia.
Kwa upande wake, Mshauri wa Rais katika masuala ya mazingira na Mwenyekiti wa AGN Dkt. Richard Muyungi amesema katika mkutano wa kwanza uliofanyika mapema mwaka huuZanzibar walikubaliana Ajenda ya nishati safi iwe agenda kubwa ya Afrika kuelekea COP30.
“Tunapopambana kuhusu mabadiliko ya tabianchi tunapaswa kuakisi hali halisi ya Afrika katikakumkomboa Mwanamke, Kijana na Mwafrika hasa kutokana na changamoto tunazozipatazinazotokana na kutokuwa na nishati safi ya kupikia pia kutokuwa na umeme.
“Umeme ni ajenda ya pili ambapo hadi kufikia 2030 asilimia kubwa wawe wanatumia umeme namwisho ni fursa kwa vijana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa vijanawengi walikuwa hawashirikishwi lakini kwa sasa tumewapa kipaumbele,” amesema Dkt. Muyungi.
Naye, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, Mhandisi UssiKhamis Debe akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,amesema asilimia kubwa ya uchumi wa Zanzibar umejikita zaidi kutokana na Uchumi wa Buluu.
Amesema Uchumi wa Buluu una maeneo mengi kwa upande wa Zanzibar kama vile Uvuvi, Kilimo, Utalii na maeneo hayo yamekuwa yakikumbwa na changamoto kutokana na mabadilikoya tabianchi.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati)akizungumza wakati wa Kikao cha Makatibu Wakuu cha maandalizi ya COP 30 kilichofanyika Dodoma Oktoba 21, 2025. Kushoto ni Mshauri wa Rais katika masuala yamazingira na Mwenyekiti wa AGN Dkt. Richard Muyungi na kulia ni Katibu Mtendajiwa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, Mhandisi Ussi Khamis Debe.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja akifungua Kikao cha Makatibu Wakuu cha maandalizi ya Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP30) utakaofanyika Brazil kuanzia Novemba 10 hadi 21, 2025. Kikao hicho kimefanyika Dodoma Oktoba 21, 2025.

PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Tanzania kwa nafasi yake ya Uenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (AGN) itaongoza na kubeba sauti ya pamoja ya vipaumbele vya Bara la Afrika wakati wa Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP30).
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema hayo JijiniDodoma Oktoba 21,2025 wakati akifungua Kikao cha Makatibu Wakuu cha maandalizi ya COP 30 utakaofanyika Brazil kuanzia Novemba 10 hadi 21, 2025.
Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,alizindua Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 (Dira 2050) Julai 17, 2025, akiithibitisha nia ya Serikali ya kuwa na maendeleo yenye ustahimilivu wa mabadiliko ya tabiahchi na kuwa taifa lenye ustawi, jumuishi na endelevu, ambapo kila sekta ya maendeleo Nchini inatakiwa kuzingatia dhana ya maendeleo endelevu.
“Mwaka huu COP30 ni ya kihistoria kwa kuwa mkutano huu utafanyika katika nchi yenye historia ya kuanzishwa kwa Mkataba husika na hivyo ajenda zitakazojadiliwa zinatarajiwa kufafanua njia na hatua za haraka hususan katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi baada ya miaka 33 ya uwepo wa Mkataba.
“Kwa Tanzania, Mkutano huu sio wa majadiliano tu bali utahusika pia katika kuongeza mashirikiano na wadau mbalimbali duniani kwa lengo la kuongeza fedha za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zitachangia katika kukuza uchumi na kuimarisha maendeleo ya Kijani Nchini.” Amesema Luhemeja.
Ameongeza katika kuhakikisha hili, Serikali imeanza kuandaa nyezo za utekelezaji vipaumbele vya Dira, na kwa sasa, Serikali ipo katika mchakato wa kukamilisha mipango miwili muhimu ambayo ni Mchango wa tatu wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchia.
Kwa upande wake, Mshauri wa Rais katika masuala ya mazingira na Mwenyekiti wa AGN Dkt. Richard Muyungi amesema katika mkutano wa kwanza uliofanyika mapema mwaka huuZanzibar walikubaliana Ajenda ya nishati safi iwe agenda kubwa ya Afrika kuelekea COP30.
“Tunapopambana kuhusu mabadiliko ya tabianchi tunapaswa kuakisi hali halisi ya Afrika katikakumkomboa Mwanamke, Kijana na Mwafrika hasa kutokana na changamoto tunazozipatazinazotokana na kutokuwa na nishati safi ya kupikia pia kutokuwa na umeme.
“Umeme ni ajenda ya pili ambapo hadi kufikia 2030 asilimia kubwa wawe wanatumia umeme namwisho ni fursa kwa vijana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa vijanawengi walikuwa hawashirikishwi lakini kwa sasa tumewapa kipaumbele,” amesema Dkt. Muyungi.
Naye, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, Mhandisi UssiKhamis Debe akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,amesema asilimia kubwa ya uchumi wa Zanzibar umejikita zaidi kutokana na Uchumi wa Buluu.
Amesema Uchumi wa Buluu una maeneo mengi kwa upande wa Zanzibar kama vile Uvuvi, Kilimo, Utalii na maeneo hayo yamekuwa yakikumbwa na changamoto kutokana na mabadilikoya tabianchi.

Mshauri wa Rais katika masuala ya mazingira na Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (AGN) Dkt. Richard Muyungi (kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja, mara baada ya Kikao cha Makatibu Wakuu cha maandalizi ya COP 30 kilichofanyika Dodoma Oktoba 21, 2025.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikatiwaliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Manaibu na Wawakilishimara baada ya kufungua Kikao cha Makatibu Wakuu cha maandalizi ya COP 30 kilichofanyika Dodoma Oktoba 21, 2025.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikatiwaliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Manaibu na Wawakilishimara baada ya kufungua Kikao cha Makatibu Wakuu cha maandalizi ya COP 30 kilichofanyika Dodoma Oktoba 21, 2025.

PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...