Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) inatumia fursa hiyo kusikiliza na kuhudumia wateja mbalimbali wanaofika katika ofisi zake, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha huduma bora na mahusiano mazuri na wadau wake. Maadhimisho haya ya kimataifa yanafanyika kila tarehe 6 hadi 10 Oktoba, yakilenga kuhimiza taasisi na mashirika kutoa huduma bora, zenye ubunifu na zenye kujali mahitaji ya wateja wao.
Katika kipindi hiki, TCAA inapokea na kushughulikia maoni, mapendekezo, na changamoto kutoka kwa makundi mbalimbali ya wateja, wakiwemo marubani, wahandisi wa usafiri wa anga, wanafunzi, na wawakilishi wa mashirika ya ndege. TCAA inaamini kupitia utaratibu huu wa kuwa karibu na wadau, Mamlaka inalenga kuboresha mifumo ya utoaji huduma na kuhakikisha kuwa kila mteja anapata huduma bora, kwa wakati na kwa ufanisi.
Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “Mission: Possible – Mpango Umewezekana,” ambapo kwa upande wa TCAA, kauli mbiu hii inadhihirisha dhamira ya kuendelea kutoa huduma bora na zenye ubunifu unaolenga kumuweka mteja katikati ya huduma zote. Kupitia maadhimisho haya, TCAA inathibitisha kujituma kwa watumishi wake katika kufanikisha malengo ya taasisi, kuongeza ufanisi wa huduma, na kudumisha utamaduni wa ubora wa huduma kwa wateja.
Aidha, maadhimisho hayo yaliambatana na mafunzo kwa watumishi wa TCAA kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutoa huduma zenye ubunifu, weledi, na zinazozingatia mahitaji ya wateja. Bila shaka, kwa TCAA – Mpango Umewezekana.
Afisa Habari na Uhusiano Mkuu TCAA, Zuhura Lwamo (katikati) akiwasikilza wadau wa usafiri wa anga waliofika kupata huduma katika ofisi ya TCAA kitengo cha taarifa za anga (briefing office) uwanja wa ndege wa Arusha.
Afisa Mtoa Taarifa za Usafiri wa anga wa TCAA kituo cha uwanja wa ndege wa Arusha, Johneudes Mwombeki (kushoto) akifafanua jambo kwa mdau wa usafiri wa anga aliyefika kupata huduma katika ofisi hiyo.
Afisa Habari na Uhusiano Mkuu TCAA, Zuhura Lwamo (katikati) akizungumza na mdau wa usafiri wa anga aliyefika kupata huduma katika ofisi ya TCAA kitengo cha taarifa za anga (briefing office) katika uwanja wa ndege wa Arusha.
Meneja wa TCAA kituo cha Uwanja wa Ndege wa Arusha Jackson Ndalu akikabidhi zawadi kama ishara ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Kaimu Meneja Uhusiano na Mawasiliano TCAA, Ally Changwila (kulia) akiwakaribisha wadau wa usafiri wa anga waliofika Makao Makuu ya TCAA kupata huduma.
Muwezeshaji Rodrick Nabe akitoa mafunzo kwa watumishi wa TCAA kuhusu namna bora ya kutuoa huduma kwa mteja ikiwa ni sehemu wiki ya huduma kwa wateja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...