MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa katika mikoa saba inayotarajiwa kunyesha kuanziq kesho.
Mvua hiyo inatarajiwa katika katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (pamoja na visiwa vya Mafia), Morogoro na Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, hali kama hiyo pia inatarajiwa kuendelea hadi keshokutwa (Jumanne) katika mikoa hiyo na kuongezeka hadi maeneo ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Mamlaka imewataka wananchi kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa zitakazotolewa ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...