Songosongo, Kilwa — Oktoba 25, 2025

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kudhihirisha dhamira yake yakuimarisha mahusiano na jamii kupitia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), baada ya kudhamini na kuendesha bonanza kubwa la michezo na upimaji wa afya bure katikaKijiji cha Songosongo, wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

Bonanza hilo limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mbio za mita fupina kuvuta kamba, likiwashirikisha wakazi kutoka vitongoji vinne vya kijiji hicho ambavyo niPembeni, Mstumai, Funguni na Makondeni.

Lengo kuu la bonanza hilo ni kuhamasisha ushiriki wa vijana na wananchi kwa ujumla katikamichezo kama njia ya kujenga afya bora, kukuza vipaji, kudumisha mshikamano wa kijamii, na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kupima afya mara kwa mara ili kutambua hali zaomapema.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi, meneja wa kiwanda cha kuchakatagesi asilia cha songosongo, Mha. Kondoro Nteminyanda, aliipongeza timu ya Newcastle yakijiji hicho kwa kutwaa ubingwa wa bonanza hilo, sambamba na kuishukuru Kamati yamichezo ya Songosongo na timu zote zilizoshiriki kwa hamasa na nidhamu ya hali ya juu.

“Michezo ni zaidi ya burudani; ni nyenzo muhimu ya kujenga afya, kukuza ajira kupitiavipaji, na kuimarisha undugu katika jamii. Michezo ni daraja linalounganisha watu ndiyomaana TPDC inaendelea kuwekeza katika programu kama hizi zinazogusa maisha yawananchi moja kwa moja,” alisema Nteminyanda.

Aidha, alisisitiza kuwa TPDC itaendelea kuwa mdau muhimu wa maendeleo ya jamii katikamaeneo yote inayofanya shughuli zake, kama sehemu ya mchango wake katika ustawi wawananchi.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji cha Songosongo, Bw. Athumani Mohamed, alitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wote wa Songosongo kwauongozi wa TPDC kwa kudhamini na kuratibu bonanza hilo pamoja na programu ya upimajiafya.

“Bonanza hili limekuwa fursa muhimu ya kuwaleta wananchi pamoja na kuonesha kwavitendo dhamira ya TPDC ya kushirikiana na jamii. ‘‘Tunatoa rai kwa wanamichezo nawananchi kudumisha amani, upendo na mshikamano, hususan tunapoelekea katika kipindicha uchaguzi mkuu,” alisema Bw. Mohamed.

Naye kiongozi wa vilabu vya mpira wa miguu vya songosongo, Bw. Hussein Mahadhi, alishukuru TPDC kwa kuandaa bonanza hilo, akieleza kuwa limeleta hamasa, burudani namshikamano kwa wakazi wa eneo hilo. Pia alitoa wito kwa taasisi na kampuni nyingine kuigamfano wa TPDC katika kuboresha huduma za kijamii na kuinua sekta ya michezo vijijini.



Dkt. Goodluck Kabanga akitoa huduma ya upimaji afya katika bonanza la Michezo  lililofanyika Songosongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...