VICTOR MASANGU, KIBAHA
Watumishi wa afya katika ngazi za zahanati, vituo vya afya na hospitali wametakiwa kuachana kabisa na vitendo vya kuwabagua wagonjwa kwa kuwatolea lucha chafu na badala yake wahakikishe kwamba wanafanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi kwa lengo la kuweza kutoa huduma bora na ufanisi mkubwa kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt. Catherine Saguti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Afya Day ambayo yamewashirikisha wauguzi na madaktari kutoka Manispaa ya Kibaha na kuongeza kwamba anaishukuru serikali ya awmu ya sita kwa kuweza kuboresha sekta ya afya pamoja na kuimarisha miundombinu ya majengo na vifaa tiba.
Catherine amesema kwamba watumishi wa afya wanapaswa kuzingatia masomo ambayo wamefundisha pindi walipokuwa chuoni kwa lengo la kuwahudumia wagonjwa.
"Ombi langu kubwa ambalo naliomba kwenu kwa watumishi wote wa afya kuanzia ngazi za zahanati,vituo vya afya na hospitali kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kutotoa lugha mbaya kwa wagonjwa,"amesema Dkt.Catherine.
Aidha amempomgeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kusaidja kuboresha sekta ya afya.
Kwa upande wake mmoja wa madakari ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Peter Lukui amebainisha kwamba katika maadhimisho hayo wamefanikiwa kutoa huduma mbali mbali za afya pamoja na vipimo kwa jamii ambapo wamewafikia kuwafikia zaidi ya wananchi 295 ikiwa pamoja na kuwapatia elimu juu ya ,masuala ya afya.
Naye Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mkoani Dkt Abdulkadri Sultan amesema kwamba maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na kutoa huduma za afya kwa ajamii, kufanya usafi katika soko la loliondo ikiwemo pamoja na kutoa huduma mbali za upimaji wa magonjwa mbali mbali.
Nao baadhi ya watumishi wa afya ambao wameshiriki katika maadhimisho hayo wamemshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan a kwa kuweza kuwawekea mazingira rafiki ya ufanyaji wa kazi ambayo imewasadia kwa kiasi kukubwa katika kutoa huduma.
Kilele cha maadhimisho ya Afya Day ambayo kwa sasa yamefanyika kwa mwaka wa tatu sasa yamekwenda sambamba na zoezi la kufanya usafi katika soko la loliondo,kuchangia damu,kushiriki katika michezo mbali mbali na kutoa huduma kwa jamii na elimu.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...