Vodacom Tanzania PLC imetangaza uzinduzi wa filamu ya “NIKO SAWA”, filamu ya kipekee ya Kitanzania inayopatikanaw kupitia VTV, programu inayokuwezesha kuangalia tamthilia na filamu mbalimbali kwa njia ya mtandao.

Hafla ya uzinduzi wa filamu hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Cinema wa Mlimani City, ikiashiria hatua muhimu katika safari ya Vodacom ya kuwaunganisha Watanzania kupitia teknolojia. 

Kupitia ubunifu wake, kampuni inalenga kuchochea mazungumzo kuhusu masuala nyeti ya kijamii kwa kutumia burudani kama njia ya kuwaelimisha wanajamii.

Filamu ya “NIKO SAWA” inaangazia kwa kina mada ya afya ya akili, eneo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likipuuzwa katika jamii.

 Ikiandikwa na kuongozwa na watayarishaji wenye kipaji kutoka Tanzania, filamu hii inasimulia hadithi ya kuvutia ya familia inayopambana na matatizo ya kifedha, changamoto za kihisia na mapambano ya kimya kimya yanayoathiri maisha ya kila siku. 

Filamu hii imezinduliwa sambamba na maadhimisho ya Mwezi wa uhamasishaji wa afya ya akili, ikisisitiza umuhimu wa kuelewa na kujali hali za watu wanaotuzunguka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Goodluck Moshi, Mkuu wa Idara ya Ubunifu wa Kidijitali wa kampuni hiyo alisema kuwa kupitia VTV, lengo lao si kuburudisha tu bali pia kuwezesha jamii huku akiongeza kuwa “NIKO SAWA” ni hadithi inayogusa maisha na hisia za watazamaji, hususan vijana, ikikumbushia kwamba afya ya akili ni muhimu sawa na afya ya mwili. 

Vodacom inaamini kwamba teknolojia na sanaa ya usimulizi zinaweza kushirikiana kuleta mazungumzo ya kweli na kuijenga jamii yenye huruma na mshikamano.Kwa upande wake, Neema Ndepanya, muongozaji wa “NIKO SAWA” alieleza kuwa hadithi hiyo imetoka moyoni huku akidadavua kwamba nia yao ilikuwa kuunda kazi ya sanaa inayozungumzia maumivu ya kimya kimya ambayo watu wengi hubeba kila siku lakini huyaweka moyoni. 

Neema aliongeza kuwa kufanya kazi na Vodacom na kushuhudia “NIKO SAWA” ikipata uhai kupitia VTV imekuwa safari ya maana na yenye kugusa hisia. Alisisitiza kuwa pale ambapo taasisi kama Vodacom zinawekeza katika hadithi za ndani, hazisaidii tu sanaa bali pia zinaponyesha jamii, zinaanzisha mazungumzo na kutoa matumaini kwa wale wanaoyahitaji zaidi.

Wateja wanaweza kufurahia maudhui ya VTV kwa kupakua bure programu ya VTV OTT kupitia Play Store au App Store. Baada ya kujisajili, watazamaji wanaweza kuchagua kifurushi cha bei nafuu kuanzia TZS 500 tu, na kufanya malipo kwa urahisi kupitia M-Pesa au njia nyingine za malipo ya simu. 

Pia, wateja wanaweza kunufaika na ofa maalum pamoja na muda wa ziada wa kutazama.

Uzinduzi wa “NIKO SAWA” unaashiria hatua nyingine muhimu katika dhamira ya Vodacom ya kujenga maisha ya kidijitali yenye maana kwa Watanzania, maisha yanayowawezesha, kuwaburudisha na kuwaunganisha katika matukio pamoja na hisia muhimu za maisha ya kila siku.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...