Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ameshauri kuwa kilichotokea Oktoba 29, kisijirudie na watanzania wote tuseme inatosha kwani sio utamaduni wetu

Msama amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu tume iliyoundwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuchunguza matukio ya vurugu za Oktoba 29, siku ya uchaguzi mkuu mwaka huu.

Tume hiyo inayoogozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Othoman Chande, ilizinduliwa na Rais Samia, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, mjini Dodoma.

Vurugu hizo ambazo hadi leo lengo lake hazijulikani, zimesababisha vifo, uharibifu wa miundombinu, mali za Serikali na watu binafsi .

Msama ambaye alikuwa mgombea Ubunge jimbo la Ukonga (CCM),amesema huu sio muda wa kunyoshena kidole kwamba nani alikosea na nani alikuwa sahihi bali ni wakati wa kutafakari na kusema imetosha.

Kwa mujibu wa Msama, Rais Dk.Samia anastahili pongezi kwa hatua anazochukua kwani ameshatoka hadharani kutoa pole kwa wafiwa, majeruhi, wananchi na wafanyabashara waliopoteza mali zao na ameunda tume kuchunguza matukio hayo ya Oktoba 29.

"Kila mmoja ameona kilichotokea Oktoba 29.Naamini kila mtu ameona tulipokosea, vijana walioandamana na kuleta vurugu, wamejifunza kitu, viongozi wetu wamejifunza kitu, wananchi na wazazi tumejifunza tulipokosea.Sasa ni wakati wa kusema inatosha, yaliyopita, yasijirudie," amesema Msama.

Kuhusu tishio la vijana kutaka kufanya maandamano mengine Desemba 9, Msama amesema hatua hiyo inapaswa kupingwa na kila Mtanzania aliyeona matukio na hasara ya vurugu za Oktoba 29.

Amesema maandamano hayo hayana tija kwa taifa kwani Rais ameshapatika, tayari ameunda serikali yake, ameunda tume huru ya uchunguzi itakayo kuja na mapendekezo yatakayopelekwa kwenye tume ya maridhiano ili kuzuia matukio hayo ya Oktoba 29, yasijirudie.

" Nawakumbusha vijana kutambua uchaguzi umepita na Rais amepatikana, vurugu zozote haziwezi kubadilisha matokeo na hazikubaliki. Tumwache Rais afanyekazi, tuiache tume ifanyekazi yake ili tupate suluhu ya kudumu kuhakikisha Tanzania inaendelea kubaki kuwa kisiwa cha amani na utulivu," alisema Msama.

Pia ametoa rai kwa viongozi wa dini kuwa makini na kauli zao kwani zinaweza kuligawa taifa badala yake waongoze ibada na sala za kuliombea taifa.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...