NA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa Chuo cha Ufundi Farahika kinachoendesha mitaala yake chini usimamizi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kimetangaza kuanza kufundisha kozi mpya nane ikiwemo ya Uhasibu.

Mkuu wa Chuo hicho kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam ndani ya Chuo Kikuu cha St John, Aliko Mmongele amesema kozi ya Uhasibu inafundishwa chini ya Bodi ya NBAA.

Mmongele amefafanua kuwa kozi nyingine mpya ambazo zitafundishwa chuoni hapo kwa gharama nafuu ni Ufundi Bomba (Pumbling), Mapishi (Catering), Masoko (Sellesmanship), Mtoa huduma kwa wateja (Customer Care), Msoma Mita za Maji (Watermeter Reading) na Business Oparator.

Amefafanua kuwa lengo la kuanzisha kozi hizo mpya ni kuwafikia vijana wengi na kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar katika jitihada za kuwainua vijana kupitia elimu ya amali inayosaidia kuliondoa kundi hilo katika utegemezi.

“Hiki ni chuo kimekuwa kikiendesha kozi mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar na sasa tumeanzisha kozi mpya zitakazofundishwa pamoja na zile zinazotolewa kwa mpango wa elimu bure.

“Ni dhahiri zitawafikia vijana wengi wenye uhitaji wa kupata mafunzo ya ufundi stadi kama ambavyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anavyosisitiza kuhusu mafunzo ya amali kuifikisha kwenye kundi kubwa la vijana ili waweze kujitengenezea ajira baada ya kuhitimu.

“Hivyo tunawakaribisha vijana wote wa kitanzania kutoka mikoa yote hapa nchini kuja kupata mafunzo haya ambayo yanaendeshwa chini ya mtaala wa Veta kwa tafsiri ya haraka maana yake uwezi kutenganisha Chuo cha Furahika na Veta, waje kwa wingi na hata wakiwa watano tunaanza na nao zipo kozi za muda mfupi na mrefu,” amasema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...