Na Janeth Raphael MichuziTv - Dar es salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesisitiza umuhimu wa kila Mtanzania kuilinda nchi yake, akisisitiza kuwa uharibifu uliofanyika Oktoba 29, 2025 ni zaidi ya maandamano, akiita vurugu hizo kama hujuma za kiuchumi.

Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu amebainisha hayo leo Jumanne Novemba 25, 2025 wakati akizungumza na Wahariri na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam, akieleza kuwa miundombinu iliyoharibiwa si mali ya serikali bali ni miundombinu yenye kutumika na Kila Mtanzania katika kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii kote nchini.

"Miundombinu hii si mali ya serikali, zahanati si mali ya serikali, barabara pia hivyo hivyo ndiyo maana hata ukinunua shati la mtoto wako mchanga, ipo sehemu unachangia miundombinu hii." Amesisitiza Dkt. Mwigulu.

Katika hatua nyingine ametaja sehemu ya uharibifu huo uliotokea Oktoba 29, 2025 kuwa ni pamoja na ofisi za serikali 756, Vituo vya mabasi ya Mwendokasi 27,kituo cha uzalishaji Maji safi na salama DAWASCO pamoja na mabasi sita yaendayo haraka Jijini Dar Es salaam.

Aidha uharibifu mwingine ni nyumba binafsi 273, Vituo vya Polisi 159, Vituo binafsi ya uuzaji wa mafuta 672, magari ya watu binafsi 1642, Pikipiki binafsi 2268, pamoja na magari ya serikali 976 ikiwemo magari ya kubebea wagonjwa na ya kutoa huduma nyingine kwa umma.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu, wahusika pia walikuwa wamepanga kuchoma kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli Jijini Dar Es Salaam, kuchoma kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi pamoja na maeneo mengine muhimu, akisema rasilimali na mali zote hizo si mali ya serikali, hivyo kila Mtanzania anawajibika kulika rasilimali hizo kwa mustakabali wa maendeleo na ustawi wa kila Mwananchi.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...