Na Janeth Raphael MichuziTv - Dar es salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mwigulu Nchembe amewasihi Watanzania kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiunga mkono Tume aliyoiunda kuchunguza vurugu za Oktoba 29, 2025.

Amesema tukio hilo limeleta msukosuko nchini, likihusisha vifo na madhara kwa baadhi ya watu, jambo ambalo linapaswa kuwa funzo kwa taifa.

Dkt Mwigulu ameyabainisha hayo leo wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

“Baada ya kumaliza uchaguzi, kulitokea vurugu ambazo zimegharimu maisha ya baadhi ya watu. Katika imani yangu, kumwaga damu ya mtu asiye na hatia ni jambo zito. Ombi langu ni kwamba kila mmoja katika dhamira yake anatamani tusirudie kamwe jambo kama hili. Linatuachia makovu yasiyopona,” amesema.

Dkt Mwigulu amesema ni muhimu Watanzania wote kuungana na Rais Samia ili kupata uhalisia wa kilichotokea kupitia tume hiyo, ambayo imeundwa na watu wenye weledi na heshima katika jamii.

“Hiki si kitu cha kawaida, si jambo jepesi. Ndiyo maana Mheshimiwa Rais ameunda tume ya watu wanaoheshimika, waliotumikia kwenye maeneo ya haki na sheria kwa muda mrefu. Tusiingie kwenye mtego wa kutaka kushusha hadhi ya kamati,” ameongeza.

Amesisitiza kuwa kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni, lakini ni vyema kutambua kuwa wajumbe wa tume hiyo ni watu wa kuaminika na wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya kisheria, hivyo wanastahili kupewa nafasi ya kufanya kazi yao bila kuingiliwa.

Aidha Dkt Mwigulu amesema Tanzania sio nchi masikini na kama kuna watu wanaimezea mate amewahakikishia kuwa Tanzania italindwa Mpaka pointi ya mwisho na wasioitakia mema watatakwza mate yao Mpaka yawakauke.

Hata hivyo Dkt Mwiguli ametoa maagizo kwa viongozi wa Serikali ngazi zote kuhakikisha watu wabaya hawawezi kujipenyeza na kuitia doa Nchi.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...