Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb), ametoa wito kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yake kwa ubunifu na ushirikiano.

Ameyasema hayo Novemba 27, 2025 alipotembelea Shirika hilo, akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Dkt Suleiman Serera pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara Bw. Sempeho Manongi, na kuzungumza na Bodi na Menejimenti ya TBS ambapo aliwaahidi ushirikiano katika kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora na salama.

Aidha, Waziri Kapinga ameisisitiza TBS kutoa huduma zenye matokeo kwa Watanzania, kwa kuzingatia maadili, uwajibikaji na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kulinda afya na kipato cha Watanzania.

Waziri Kapinga ameiagiza TBS kuanzisha Programu za uelimishaji wa Viwango kwa wananchi na kuhakikisha mifumo inasomana ndani ya taasisi na nje ya taasisi ili kudhibiti ubora wa bidhaa kwa Kushirikiana na FCC.

Amesisitiza TBS kukamilisha miradi kwa wakati ili kuboresha huduma na kuongeza ufanisi, akitaka wakandarasi wasimamiwe ipasavyo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amesisitiza Menejimenti hiyo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi ili kutekeleza majukumu ya Shirika hilo kwa ufanisi.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBS Bw. Hussein Sufian ameahidi kuwa Bodi hiyo iko tayari kupokea na kutekeleza Maelekezo hayo kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya sita.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Ashura Katunzi amebainisha kuwa Shirika limepokea maelekezo ya Waziri na litaendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara zingine nchini ili kuhakikisha shughuli zinatekelezwa kwa ufanisi.


































Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...