Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameshiriki Mkutano wa 7 wa Viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya (AU-EU Summit), uliofanyika  Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 25 Novemba 2025.

Mkutano huo uliofanyika kwa Siku mbili, pamoja na mambo mengine umehitimishwa kwa dhamira ya kuunda mustakabali mwema na endelevu wa Afrika na Ulaya, ushirikiano mpya na imara juu ya amani, usalama na utawala katika kukabiliana na vita na migogoro kote ulimwenguni.

Masuala mengine yaliyopewa kipaumbele katika Mkutano huo ni pamoja na ahadi madhubuti ya ushirikiano wa kimataifa pamoja na ushirikiano imara na wa kuheshimiana katika masuala ya uhamiaji na uhamaji.

Mkuatano huo pia umedhamiria kuendelea kusaidia nchi zote za Kiafrika katika maendeleo, viwanda, kuongeza mauzo ya nje, na kuunganisha katika masoko ya kikanda. Pia makubaliano yamefanyika katika nia ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA).

Pia kukuza maendeleo endelevu kwa kuzingatia minyororo ya thamani kwa kuongeza uwezo wa viwanda vya ndani kushiriki katika masoko ya kikanda na kimataifa, ikiwemo uongezaji thamani wa madini adimu.

Ili kuwezesha biashara, Mkutano huo, umesisitiza umuhimu wa kudumisha uwazi, na njia zinazojumuisha mazungumzo, ikijumuisha biashara na shughuli za kimazingira, na kukuza ushirikiano kupitia kujenga uwezo na usaidizi wa kiufundi ili kusaidia nchi za Kiafrika kuondoa kaboni na kusimamia rasilimali asilia kwa njia endelevu.

Mkutano huo umedhamiria kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na kukuza uendelevu wa mazingira, kwa kutatua changamoto pamoja zinazoletwa kwa wauzaji bidhaa kutoka Afrika kwa njia endelevu.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo umeadhimisha miaka 25 ya ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.

Mkutano huo umefanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Kukuza amani na ushirikiano kupitia Ustawi wa Kimataifa wenye Tija” (promoting peace and prosperity through effective Multilateralism)

Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kazi na Uwekezaji Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Sharif Sharif, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Ngwaru Maghembe, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Afrika Mhe. Balozi Innocent Shiyo, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Umoja wa Ulaya Mhe. Balozi Jestas Nyamanga, pamoja na wataalamu mbalimbali.

 

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

25 Novemba 2025

Luanda - Angola.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...