Makumbusho ya kisasa ya Jiopaki ya Ngorongoro-Lengai (Urithi Geo Museum) iliyoko Karatu Mkoani Arusha ni zao jipya la utalii ambapo pamoja na mambo mengine inatoa fursa ya kujifunza historia ya sayansi na mazingira kwa wanafunzi wanaotembelea makumbusho hiyo.

Wadau mbalimbali wameendelea kutembelea makumbusho hiyo ambapo leo tarehe 19 Novemba, 2025 wanafunzi na walimu  kutoka shule ya Msingi Paradise iliyopo Chato Mkoani Geita wamepata elimu  kuhusu muonekano wa dunia kwa miaka mingi iliyopita na ilivyo sasa, maumbile asilia yanayopatikana katika ukanda wa bonde la ufa, kujionea mwamba wenye umri wa miaka milioni tatu iliyopita unaopatikana hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai, kujifunza tamaduni za makabila ya  Wahadzabe, Wairaqw, Wadatoga na Wamasai pamoja, kupima uwezo wa kutambua sauti za wanyamapori, kushindana mbio kwa kutumia baiskeli na wanyamapori  ndani ya makumbusho.

Fursa zitakazotokana katika makumbusho hiyo ya kisasa ni pamoja na kuongeza zao jipya la utalii wa jiolojia na miamba, ukuza utafiti wa kisayansi na elimu ya kijiolojia, kuwezesha jamii na wanafunzi kujifunza historia ya sayansi na mazingira, kuongeza ajira na kipato kwa wananchi wa maeneo jirani na kuimarisha nafasi ya Tanzania kimataifa kama kinara wa uhifadhi, utalii na kielimu.

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro lilipewa hadhi ya kuwa eneo lenye utalii wa Miamba “Geopark” mwaka 2018  na kuwa Jiopaki pekee katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara na ya  pili kwa Afrika ikitanguliwa na Morocco.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...