Na Mwandishi wetu – Dodoma

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Hamad Chande (Mb) ameitaka menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa ushirikiano katika kutimiza ndoto za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulijenga Taifa.

Ameyasema hayo katika kikao na menejimenti ya Wizara hiyo kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma Novemba 18,2025 mara baada ya kuripoti ofisini hapo.

“Rais Samia amesema miradi tunayoihitaji kutekeleza ni mingi muda ni mchache na ndani ya siku 100 yako mambo anayotaka tuwe tumeyafikia hivyo sisi hatuwezi kuyafikia bila uwepo  wenu ninyi kwa taaluma zenu na mashirikiano yenu ya dhati kwetu” amesema Mhe. Chande.

Pia ameitaka menejimenti hiyo kutekeleza falsafa ya  “Ishi vyema na watu ,Ufanye kazi kwa utu, Uwatambue watu ili na wewe uwe mtu mbele za watu”.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...