MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amekula kiapo cha Uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Musa A. Zungu, tarehe 11 Novemba, 2025. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kuwa Mbunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi na tatu(13) wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inayompa Mamlaka ya kuwa Mbunge na kuhudhuria vikao vya Bunge.

Aidha, Uapisho huo mbele ya Bunge wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, unafuatia Uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kumteua Mhe. Hamza S. Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mnamo tarehe 3 Novemba, 2025 na kufuatiwa na uapisho uliofanyika tarehe 5 Novemba, 2025 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...