Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeendelea na juhudi zake za kuwawezesha wakulima kupitia mafunzo ya uelewa kuhusu huduma na bidhaa zake kwa wakulima 120 kutoka Wilaya za Songea Mjini, Songea Vijijini, Namtumbo pamoja na Madaba mkoani Ruvuma.

Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Brig. Gen. Ahmed Abbas Ahmed, ambaye aliwahimiza washiriki kutumia maarifa waliyopata kuboresha uzalishaji, kuongeza tija, na kuimarisha ufanisi katika shughuli zao za kilimo-biashara.

Miongoni mwa mada kuu zilizojadiliwa katika mafunzo hayo ni:

. Huduma na bidhaa za TADB

. Urasimishaji wa kilimo-biashara

. Mfuko wa Dhamana ya Mikopo kwa Wakulima Wadogo (SCGS)

. Hali ya kilimo, ufugaji na uvuvi katika Wilaya ya Songea Mjini

Uimarishaji wa vyama vya ushirika na AMCOS.

Washiriki wa mafunzo walihusisha:

1. Vikundi vya wakulima kutoka Nakaheguo Group, Nalima AMCOs, Lumbingu Farmers, Juhudi Mpitimbi Farmers, Luganga Farmers, Ngoni Organized Farmers Group, na Umatengo Farmers Group.

2. ⁠Wakulima binafsi kutoka maeneo ya Mtyangimbole, Mbinga Muhalule, Litisha, Nakahuga, Matomondo, Msamala, Namtumbo, na Mshangano.

3. ⁠Wajasiriamali wa Ruvuma Mwalu.

Wakulima walioshiriki walitoa shukrani zao kwa TADB kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu, wakisisitiza kuwa yamewapanua uelewa kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na benki hiyo, na jinsi wanavyoweza kunufaika nazo ili kukuza shughuli zao za kilimo-biashara.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...