NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZ TV

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetamba kuwa litaibuka kidedea katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) 2025 ambayo yanaendelea mkoani Morogoro.

TBS imedai kuwa maandalizi yao ya takribani mwaka mzima yamewaweka katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri katika michezo yote wanayoshiriki, ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, mpira wa wavu kwa wanaume na wanawake, kuruka kamba pamoja na michezo ya jadi ya ndani kama karata, drafti, pool table, bao na vishale.

Wanamichezo wa shirika hilo, wakizungumza na waandishi wa habari, wamesema wamejidhatiti kuhakikisha TBS inafanya vizuri na kushindana kwa ushindani mkubwa katika kila mchezo.

Aidha, wamesema mashindano ya SHIMMUTA ni chachu ya kujenga afya, kuongeza umoja, na kuimarisha mahusiano baina ya taasisi pamoja na jamii ambako TBS hupata nafasi ya kujitangaza zaidi.

“Kupitia michezo tunalitangaza shirika letu, tunajenga afya na tunaimarisha mahusiano ya kijamii na kitaasisi. Michezo ina faida nyingi kuanzia kwa mtu binafsi hadi serikali,” wamesema.

Mashindano ya SHIMMUTA hufanyika kila mwaka yakilenga kuimarisha uhusiano chanya wa kitaasisi kupitia ushiriki wa michezo mbalimbali.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...