Timu ya mpira wa Netiboli na mpira wa wavu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewasili mkoani Morogoro tarehe 25 Novemba 2025, imeendelea na program ya mazoezi katika viwanja vya Bwalo la JKT ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya SHIMMUTA ambayo yameanza tarehe 25 Novemba, 2025.
Akizungumza wakati wa mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo yanayohusisha timu za mashirika mbalimbali, kocha wa timu ya Ngorongoro, Mathias Evarist ameeleza kuwa wachezaji wako tayari kuonyesha uwezo wao na kupambana katika michezo iliyoanza tarehe 25 Novemba hadi 06 Desemba 2025.
Kwa mujibu wa Afisa Michezo Mwandamizi wa NCAA Bw. Yotham Gitige, katika mashindano hayo Ngorongoro inashiriki michezo ya mpira wa Netiboli, Mpira wa wavu na mchezo wa Riadha.



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...