Ikiongozwa na falsafa ya Mteja Kwanza huku ikizingatia Ubora wa Biashara
Dar es Salaam, Tanzania – 26 Novemba 2025: Vodacom Tanzania PLC leo imezindua msimu wa sikukuu kama kipindi cha kusherehekea na Jamii, huku ikihitimisha sherehe za kumbukumbu ya miaka 25 ya huduma tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. Kupitia kampeni hii, Vodacom inathibitisha ahadi yake ya Tupo Nawe Tena na Tena kwa kushirikiana na wateja moja kwa moja kwa kusherehekea, kuwazawadia na kusambaza furaha katika jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Philip Besiimire, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Vodacom Tanzania PLC, alisisitiza dhamira hii, akibainisha kuwa mpango huu si tu kuhusu furaha ya sikukuu bali pia kuimarisha mahusiano na kuboresha uzoefu wa wateja kama sehemu ya dhamira pana ya Vodacom ya kuwaleta wateja karibu na kuleta maendeleo ya pamoja.
“Vodacom imebadilisha maisha kupitia mtandao wake mpana na ubunifu. Msimu huu wa sikukuu, tunasherehekea wateja, washirika na jamii zinazofanikisha safari yetu,” alisema Bw. Besiimire, akiongeza kuwa Vodacom inabaki kuwa mtandao bora unaowaunganisha watu na wapendwa wao katika msimu huu wa sikukuu (Mtandao Supa Unaokuunganisha na Uwapendao).
Kwa upande wake, Brigita Stephen, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko (CBU), alibainisha kuwa kampeni hii itasambaza makapu 600 ya sikukuu yaliyojaa mahitaji muhimu ya msimu huu, sambamba na ofa maalum kwa wateja wanaolipia kupitia M-Pesa katika maeneo mbalimbali.
“Kampeni yetu ya sikukuu inalenga mteja kwanza, ikimaanisha unafuu, urahisi na thamani. Kupitia mpango wa Makapu, tunarudisha kwa jamii huku tukisherehekea wateja wetu ambao wamekuwa nasi siku zote,” alieleza, akiongeza kuwa mpango huu unathibitisha nafasi ya Vodacom kama chapa yenye uwajibikaji wa kijamii.
Akiunga mkono juhudi hizi za kurejesha kwa jamii katika msimu huu, Epimack Mbeteni, Mkurugenzi wa M-Pesa, alitangaza ofa za kuvutia za sikukuu, ikiwemo punguzo la kati ya asilimia 50 hadi 100 kwenye tiketi za SGR katika baadhi ya siku, mafuta lita mbili bure katika vituo vilivyochaguliwa na mpango wa kurejeshewa (Cashback) hadi asilimia 10 ya ulicholipia kwenye maduka makubwa na maeneo ya huduma za chakula na malazi (HoReCa).
“M-Pesa inafanya malipo ya sikukuu kuwa rahisi na yenye faida zaidi. Kupitia mafuta ya bure na marejesho ya asilimia 10, tunaongeza urahisi na kuimarisha mfumo wa malipo ya kidijitali hapa nchini,” alisema Mbeteni.
Kwa upande wa ofa za kwa wafanyabiashara wa chini na wa kati, Nguvu Kamando, Mkurugenzi wa Vodacom Business, alifichua punguzo kwa Kundi hilo, ikiwemo punguzo la asilimia 15 kwenye bei za vifurushi vya jumbe fupi (SMS) kwa wingi, miezi miwili ya usajili wa bure kwa ufuatiliaji wa magari na punguzo la asilimia 20 kwenye vifaa vya ufuatiliaji wa magari.
“Vodacom Business inawezesha biashara na watu binafsi wakiunganishwa kupitia ofa maalum za sikukuu,” alihitimisha Kamando.
Kampeni ya msimu huu wa sikukuu ya Vodacom Tanzania inasisitiza dhamira yake ya kuunganisha watu na kuwezesha maendeleo. Kupitia ofa zilizobuniwa maalum kwa ajili ya huduma za wateja, kifedha na biashara, Vodacom inaendelea kusherehekea wateja huku ikiboresha mustakabali wa kidijitali wa Tanzania.


.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...