NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ameutaka uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuongeza juhudi katika kufanya utafiti wa kubaini vivutio vipya vya utalii, ili kuimarisha ushindani na kuongeza idadi ya watalii nchini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisi za TTB, Dkt. Kijaji amesema Tanzania imejaaliwa kuwa na vivutio vingi, hivyo ni muhimu kufanyika kwa tafiti za mara kwa mara ili kugundua maeneo mapya yatakayoongeza mvuto kwa watalii.

“Malengo ya Ilani ya CCM ni nchi kupata watalii milioni nane. Lazima mjikite kwenye utafiti na kubaini vivutio vipya vitakavyotusaidia kutimiza malengo haya,” amesema Dkt. Kijaji.

Aidha, Waziri huyo ameitaka Idara ya Masoko ya TTB kuchambua changamoto inayowakumba baadhi ya watalii ambao wanakuja nchini lakini hawarudi tena mara baada ya kuondoka, akisisitiza umuhimu wa kuboresha uzoefu wa watalii ili kujenga utamaduni wa kurejea na kuwaleta wageni wengine

“Tunataka mtalii akiondoka arudi tena nchini, na pia awe balozi wetu kwa kuwaleta wageni wengine,” amesema.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kijaji ameitaka TTB kutumia fursa ya michezo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), ambayo Tanzania ni mwenyeji, kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ili kuhamasisha wageni watakaokuja nchini kushiriki pia katika shughuli za utalii.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...