Na Mwandishi Wetu

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua kifurushi cha huduma ya Faiba Mlangoni kwako kwa ajili ya kumuwezesha mteja kupata huduma ya Internet yenye kasi kwa gharama nafuu.

Kifurushi hichi ni bora na Uhakika wa huduma hiyo popote ulipo saa 24/7 kinachopatikana kwa gharama nafuu kuanzia 70,000 kwa mwezi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kifurushi cha huduma ya Faiba Mlangoni kwako Meneja Promosheni wa TCCL Janeth Maeda amesema huduma ya kifurushi hicho ni safari ya Shirika katika kuboresha na kuimarisha mawasiliano ya kidijitali nchini.

Amesema dunia ya sasa inaendeshwa kwa nguvu ya teknolojia na mawasiliano kwa kutumia Intaneti ya kasi na huduma za mawasiliano zinahitajika si tu kwa starehe, bali ni sehemu ya maisha ya kila siku — nyumbani, shuleni, ofisini, na pamoja na biashara ambapo ndipo eneo la TTCL limewekeza zaidi, kuhakikisha huduma za mawasiliano nchini zinakuwa imara, za uhakika na kwa gharama nafuu.

Janeth amesema kupitia uwekezaji huo wanalenga kufikisha huduma za kisasa hadi katika makazi ya watu, Ofisi na biashara pamoja kuunganisha Watanzania wote bila kujali wanapoishi.

Aidha amesema TTCL, imeendelea kusikiliza kwa makini maoni, mahitaji, na matarajio ya Watanzania kutoka kila pembe ya nchi katika kuhudumia mawasiliano yaliyo bora.

"Tumejifunza kwamba, wananchi wanahitaji huduma rahisi kutumia, za gharama nafuu, lakini zenye ubora wa juu itakayotoa tafsiri ya thamani halisi kwa fedha wanazotumia katika harakati za kuboresha maisha yao"amesema Maeda

Janeth alibainisha kuwa kifurushi kipya kinajumuisha huduma tatu za kifurushi kimoja bili moja ambazo ni Intaneti (Unlimited Internet) kwa matumizi ya familia, ofisi, biashara, na hata mifumo ya kidigitali Huduma ya Simu ya Mezani (Landline Voice Service) inayompa mteja fursa ya kupiga na kupokea simu kwa urahisi kupitia miundombinu ya Faiba,Huduma ya Intaneti na Dakika kwa Simu ya Mkononi (Mobile Services) inayomwezesha mteja kupata vifurushi vyenye GB na Dakika za kutosha ambavyo vinaweza kutumika popote pale mteja alipo akiwa na Laini ya simu ya TTCL, na anaweza kuwaunganisha ndugu na jamaa au wafanyakazi wake na kufurahia spidi ile ile .

Amesema TTCL ni ya kwanza Tanzania kutoa kifurushi hicho kinachojumuisha huduma tatu kwa kwa pamoja “T.Fibre Triple Hub” lengo likiwa ni kuunganisha Watanzania wote kwa njia bora, rahisi na ya kisasa kwa gharama nafuu.

Shirika pia linalenga kuhakikisha kila nyumba, kila ofisi, na kila Mfanyabiashara hapa nchini anakuwa sehemu ya mageuzi haya ya mawasiliano na hivyo kuunga mkono agenda ya serikali ya kuongeza matumizi ya TEHAMA na kukuza uchumi kidigitali.

Amesema Kifurushi kipya kimeundwa kwa ajili ya wateja wa familia, taasisi, pamoja na mteja yeyote anayehitaji ubora na urahisi katika huduma za mawasiliano.Faida ya Kifurushi cha Faiba Mla ngoni Kwako “T.Fibe Triple Hub” ni Kifurushi kwa Wateja wote.

Mteja anapata manufaa makubwa ya Intaneti ya kasi kubwa bila kikomo (Unlimited Internet), yenye uwezo wa hadi 20 Mbps upload na 20 Mbps download – intaneti imara, ya uhakika, inayokidhi mahitaji ya nyumbani, kazini, na biashara.Dakika 300 za mawasiliano, ambazo unaweza kutumia kupiga simu za mezani na simu ya Mkononi.GB 20 za intaneti kwa simu ya mkononi, ambazo unaweza kutumia popote ulipo na hata kushirikiana na familia yake.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...