Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kushiriki kongamano la Biashara baina ya Makampuni ya Tanzania na Waagizaji Bidhaa kutoka Korea- KOIMA lililoangazia kuimarisha ushirikiano yakinifu wa biashara kwa kuzingatia Maendeleo ya Biashara na Uchumi baina ya nchi hizo mbili,

Dkt. Latifa M. Khamis Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade akizungumza kwa upande wa Tanzania ameainisha mambo mbalimbali ikiwemo, kuhamsisha wafanyabiashara wa Tanzania kuchukua fursa za Biashara zinazohitajika Korea Kwani Makampuni 15 yaliyokuja ni makubwa nchini humo na hununua bidhaa kwa zenye ubora na kiwango cha juu zenye thamani ya zaidi ya USD milioni 700 kwa mwaka,

Hivyo ametoa Rai kwa wazalishaji wa Tanzania kuhakikisha wanasajili bidhaa zao na alama rasmi ya Made in Tanzania ili kuweka urahisi kufanya biashara kwenye masoko ya kimataifa na pia alichukua nafasi hiyo kuwakaribisha kushiriki kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026),

Kutangaza bidhaa za kilimo ambazo ni Made in Tanzania, hususan kahawa na bidhaa nyingine, ili kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinatambulika vyema kwenye masoko ya Korea.

Nchi hizi mbili zinafanya biashara katika sekta za Kilimo, Madini, Pamba, Mchele, Korosho, vipodozi, Teknolojia nk.

Aidha, kupitia Kongamano Hilo, Tanzania na Korea zimeingia mkataba wa makubaliano ya Biashara kupitia Sekta Binafsi (Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na (Korea Importers Association- KOIMA) ili kushirikiana kibiashara.

Kongamano hilo limezinduliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...