Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amekipongeza Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kwa kazi kubwa ya kuwaandaa vijana kujitegemea kwenye masuala ya biashara.

Alitoa pongezi hizo alipotembelea chuo hicho jana kwaajili ya kujitambulisha katika mwendelezo wa ziara zake katika taasisi zilizo chini ya wizara yake.

Alikipongeza chuo hicho kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa jengo la metrolojia ambalo ujenzi wake wa awamu ya kwanza umefikia asilimia 80 ya ujenzi wake

Alisema miradi yote ya chuo iendelee kutekelezwa kwa weledi na ufanisi mkubwa na kuhakikisha inakamilika ndani ya muda wa mkataba uliosainiwa ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

“Kwa kuwa miradi hii ni kwaajili ya kuongeza ufanisi basi sisi tunapenda ikamilike kwa haraka ili yale ambayo tunategemea yatatimia baada ya miradi hiyo basi yatimie, nimeona video nzuri ya CBE na nimesikiliza maelezo ya uongozi wa chuo nasisi tunamipango yetu kama Dira ya 2050 tunataka itekelezwe,’ alisema

Waziri alisema kwenye dira ya 2050 serikali imepanga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kati ya uchumi wa viwanda utakaoiwezesha kujitegemea na kufikia dola trilioni moja.

Alisema Tanzania inapanga kuwa miongoni mwa nchi tatu Afrika zinazoongoza kwa kuvutia uwekezaji na kwamba dira ya maendeleo inasisitiza uchumi shindani na bunifu na uwekezaji mkubwa kwenye rasilimali watu.

Aidha, alisema hakuna namna ya kufikia malengo yaliyoko kwenye Dira ya taifa kama hakuna vyuo imara vyenye kutoa elimu bora ya biashara na fedha kama chuo cha CBE.

Alisema CBE inatarajiwa kuwa itakuwa mhimili wa utekelezaji wa vipaumbele vya sekta ya baishara vilivyomo kwenye Dira ya taifa ya 2050 kwa kutoa elimu ya taaluma mbalimbali yenye tija kwa kwa vijana.

“Naiona CBE kama kiwanda cha maarifa ambacho kinazalisha wataalamu bora wa biashara, masoko, na teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na kama hatufanyi hivyo naamini tunapaswa kufanya mabadiliko ili tuendelee kuwa kiwanda cha maarifa,” alisema

“CBE inapaswa kuwa kiwanda cha maarifa kwa wizara yetu, chuo kinachotoa tafiti mbalimbali, kwasababu miminaamini nyinyi ndiyo kiwanda cha maarifa cha wizara mtakuwa wachambuzi wa sera wa Wizara kwasababu mna rasilimali za kutosha, tukitaka sera au uchambuzi wa sera tunakuja CBE” alisema Waziri Kapinga

aMkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, alisema CBE imejipambanua kwenye kutoa tafiti zinazolenga kutatua changamoto za jamii na kuchangia maendeleo ya viwanda na biashara.

Alisema chuo kimeweka utaratibu wa kutenga rasilimali za ndani kugharamia tafiti mbalimbali zinazofanywa na wahadhiri na watafiti wa chuo hicho .

Alisema katika miaka mitano iliyopita wataalamu wa CBE wamekamilisha tafiti 418 na kuchapisha zaidi ya machapisho 447 katika majarida ya kitaifa na kimataifa.

Profesa Lwoga alisema takwimu hizo zinaonyesha wazi ubora na uzalishaji wa kisayansi wa chuo hicho na mchango wake kwa serikali katika kutatua changamoto za kisera, kiuchumi na kijamii.

“Mfano dhahiri wa mafanikio katika eneo hili ni mkutano wa wa kitaaluma wa mwaka 2025 uliofanyika mkoani Dodoma uliokusanya watafiti, na wanataaluma kutoka ndani nan je ya nchi kuwasilisha matokeo ya tafiti zao kuhusu ustahimilivu wa uchumi na biashara kwa maendeleo jumuishi,” alisema 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...