📌Atembelea mradi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera

📌Awaasa wananchi kutunza mazingira ili kulinda vyanzo vya maji.

📌Zaidi ya Bilioni Kumi zimetumika kutekeleza miradi hii.


Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba leo Novemba 26, 2025 ametembelea na kukagua mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maji la Bwala la Mtera liliopo mpakani kati ya Iringa na Dodoma, ambapo amesema kuwa wananchi wa mikoa ya Dodoma na Iringa sasa kuwa na umeme wa uhakika.

Mhe. Makamba amesema Mitambo ya kufua umeme imeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana na mitambo hii inauwezo wa kuzalisha umeme mpaka ifikapo msimu ujao wa mvua na hii ni habari njema kwa wananchi wa wilaya ya Mpwapwa,Chamwino na Isimani .

“ Kimsingi mitambo hii mara baada ya kuboreshwa inatuhakikishia kuwa umeme unapatikana wa kutosha hivyo kwa ujumla mikoa ya Dodoma na Iringa itakuwa na umeme wa uhakika".Alisema Mhe. Makamba

Aidha Mhe Makamba aliongeza kuwa juhudi hizi za Serikali lazima tumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amehakikisha anasikiliza changamoto za wananchi na kuzitatua.

Amesema hadi kukamilika kwa mashine hizi mbili jumla ya zaidi ya shilingi Bilioni Kumi zimetumika katika kurekebisha na kutengeneza mitambo hii ya kuzalisha umeme.

Sambamba na hilo Mhe. Makamba ametoa rai kwa wananchi wanaozunguka vyanzo vya maji ambavyo ni chanzo cha Bwawa la Mto Mtera ikiwemo wananchi waishio pembeni mwa bonde la Ihefu kulinda vyanzo hivyo kwa sababu nishati ni uti wa ngongo wa uchumi wa Tanzania.

Kwa Upande wa Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji wa umeme TANESCO Mha. Athanasius Nangali ameeleza kuwa kituo kinafanya kazi vizuri na kituo hiki kinaendelea kuzalisha Megawati 80 kama ilivyokuwa awali.

Amewataka Wananchi waendelee kuwekeza katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kutokana na umeme unapatikana kwa uhakika na hii inatokana na kukamilika kwa kituo cha kupokea na kupoza umeme kipya kilichojengwa kutokana na usimamizi wa wakala wa nishati vijijini (REA).










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...