Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein akimtunuku Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Dkt. Juma Homera, Shahada ya Uzamivu (PhD) katika mahafali ya Chuo Kikuu Mzumbe yaliyofanyika leo Novemba 20 katika Kampasi Kuu ya Morogoro.

=====  ======  ====

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Dkt. Juma Homera, ametunukiwa rasmi Shahada ya Uzamivu (PhD) katika mahafali ya Chuo Kikuu Mzumbe yaliyofanyika leo Novemba 20 katika Kampasi Kuu ya chuo hicho, Morogoro.

Dkt. Homera alifanya tasnifu ya “Institutional Context of the Village Land Councils and the Land Use Conflict Between Farmers and Pastoralists in Tanzania.”

Utafiti huu umejikita kuchunguza mazingira ya kiutawala na kiutendaji ya Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji (Village Land Councils) na namna taasisi hizi zinavyokabiliana na changamoto za migogoro ya matumizi ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, mojawapo ya changamoto kubwa zinazolikabili taifa katika maeneo ya vijijini.

Tasnifu hiyo inatoa mchango muhimu katika kuboresha utendaji wa vyombo vya ardhi ngazi ya kijiji, kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji, na kuimarisha usimamizi wa ardhi kwa mujibu wa sheria na utawala bora.

Tasnifu hiyo ilisimamiwa na Prof. Henry Mollel pamoja na Dkt. Gustav Kunkuta.

Mhe. Homera ni miongoni mwa wahitimu 15 waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu mwaka huu Chuo Kikuu Mzumbe, wakiwemo wanaume kumi na wanawake wanne.

Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe umeeleza kuwa idadi hiyo inaonesha ukuaji wa uwekezaji katika taaluma za juu, utafiti na ubunifu nchini, hatua muhimu katika kuchochea suluhisho la changamoto za kijamii kupitia tafiti zenye tija.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...