Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea Kitabu Maalum chenye habari picha kutoka kwa Mkurugenzi wa Tahsil Solutions, Benny Kisaka, ambacho kina mkusanyiko wa taarifa za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar 2025 leo tarehe 20 Novemba 2025 Ikulu Zanzibar,

Dkt. Mwinyi amempongeza Mkurugenzi huyo kwa ubora na umakini uliotumika katika kukusanya taarifa na kutengeneza kitabu hicho.

Mkurugenzi wa Tahsil Solutions, Benny Kisaka, amefika Ikulu Zanzibar leo tarehe 20 Novemba 2025 kwa ajili ya kumkabidhi Rais Dkt. Mwinyi kitabu hicho, ambacho baadaye kitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akipokea Kitabu Maalum chenye habari picha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Tahsil Solutions, Benny Kisaka (kushoto), ambacho kina mkusanyiko wa taarifa mbalimbali za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar 2025, leo tarehe 20 Novemba 2025 Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Tahsil Solutions, Benny Kisaka (kushoto), kuhusu Kitabu Maalum chenye habari picha kutoka kwa (kushoto), ambacho kina mkusanyiko wa taarifa mbalimbali za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar 2025, leo tarehe 20 Novemba 2025 Ikulu Zanzibar. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar, Raqie Mohammed Hashim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...