Katibu Mtendaji wa Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika wa Kujitathmini kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) Tanzania, Bw. Lamau Mpolo, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Lengo la kikao hicho lilikuwa kujadili nafasi ya vijana katika kukuza dhana ya Utawala Bora kama nguzo muhimu ya kuimarisha amani na usalama nchini Tanzania.
Katika kikao hicho, Bw. Mpolo alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa vijana katika masuala ya utawala, akieleza kuwa vijana ni rasilimali muhimu katika kujenga jamii yenye uwajibikaji, uwazi na maamuzi jumuishi.
Kikao hicho cha siku moja kilifanyika Desemba 22, 2025, katika Ofisi za APRM zilizopo katika jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...