15 Disemba, 2025.
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua rasmi minara 5 katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkuranga, Kilimanjaro, Dodoma, Karatu, na Simiyu. Minara hii ni sehemu ya mkakati wa airtel wa kupanua wigo na kuweza kuwafikia watanzania wengi waishio maeneo ya mijini na vijijini.
Wakizungumza katika nyakati tofauti Mameneja wa kanda ya Mikoa ikiwemo Mkoa wa Dodoma Bw. Salum Ngururu, Amesema kuwa “Sote tunatambua umuhimu wa Mawasiliano katika jamii yetu, Hivyo Airtel tumeamua kupanua wigo wetu wa mawasiliano na kuweza kuwafikia nyie ndugu zetu mnaoishi hapa Kizota, Dodoma. Mnara huu utarahisiha upatikanaji wa huduma zetu za Airtel ikiwemo kupiga, Kutuma na kupokea pesa, pamoja na kufurahia interneti yetu yenye kasi ya 4G na 5G.
Nae Meneja kanda wa Mkuranga, Kimanzichana, Bw. Lusajo Mwakapeje, alieleza kuwa Wakati Mwingine wanakijiji walikuwa wanapata shida kuwasiliana na jamaa zao, kwasababu wakiwa katika maeneo haya ya tambalale mtandao unakuwa haushiki kabisa, Aliongeza kwa kuishukuru kampuni ya Airtel kwa Kujenga mnara wa mawasiliano kijijini hapo.
Naye Meneja wa kanda Airtel Karatu, Bw. Kephar Kileo, Akizungumza na wananchi wa Karatu amesema “kuwa Kadri uhitaji wa mawasiliano unavyozidi kuongezeka hasa ukichangiwa na ukuaji wa kidigitali, ndivyo na sisi Airtel tunavyoongeza wigo wa mawasiliano kwa kujenga minara katika maeneo ambayo yanauhaba wa miundombinu ya mawasilianoa kama ilivyokuwa hapa Karatu.”
Minara hii ya mawasiliano itachangia kufungua fursa kwa vijana, akina mama na watu wote walipo katika mnyororo wa shughuli za kibiashara, Mikoa hii iliyopo kanda inaongoza kwa ufugaji pamoja na kilimo, shughuli hizi zote zinategemea mawasiliano katika kuwaunganisha wazalishaji na wanunuzi au Masoko. Hivyo uwepo wa minara ya mawasiano ya Airtel unaenda kufungua rasmi mzunguko mkubwa wa kibiashara na uzalishaji Tanzania.
Kadhalika meneja wa kanda Simiyu Bw. Fernand Doya, Ambaye katika kanda yake wamezindua minara miwili huko Masewa bariadi vijijini na Kilalo Simiyu vijijini, alizungumza na wananchi wa maeneo hayo akisema “Airtel tumejidhatiti katika kuhakikisha tunajenga minara mingi zaidi hata katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi, ili ukuaji wa kidijitali usimuache mtu nyuma. Tuna minara takribani 200 ambayo itazinduliwa msimu huu katika kata mbalimbali za kila mkoa hapa nchini, lengo likiwa ni kusogeza huduma zetu karibu na wateja wetu.”
Uzinduzi huu uliambatana na ofa maalum ya siku tatu kwa wakazi wanaotumia minara hii, ambapo Airtel iliwawezesha kupata dakika 50 za kupiga mitandao yote, MB 500 za intaneti pamoja na SMS 50 ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa wananchi wa maeneo hayo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...