Exim Bank Tanzania imezindua rasmi kampeni yake ya miezi miwili ya matumizi ya kadi msimu wa sikukuu, iitwayo ‘Chanja Kijanja, Dili Ndio Hili.’ Kampeni hii, inayofanyika kuanzia 1 Desemba 2025 hadi 31 Januari 2026, inalenga kuwahamasisha wateja kutumia malipo yasiyotumia fedha taslimu na kuwazawadia wale wanaotumia kadi za Exim Mastercard kupitia mashine za POS na mifumo ya malipo mtandaoni katika kipindi cha ongezeko la matumizi ya ununuzi wa sikukuu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi katika Benki ya Exim Andrew Lyimo, alisema kampeni hii inaonyesha dhamira ya benki kutoa huduma rahisi, salama na zenye manufaa kwa wateja wanaotumia mifumo ya malipo ya kidijitali.
“Kupitia ‘Chanja Kijanja, Dili Ndio Hili’, tunataka kufanya malipo ya kila siku kuwa rahisi zaidi huku tukiwapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali katika msimu huu wa sikukuu. Mpango huu unaakisi kujitoa kwetu, kukuza utamaduni wa malipo ya kidigitali na kuboresha uzoefu wa wateja kote nchini,” alisema.
Zawadi kwa Washiriki:Zawadi za Kila Wiki: Wateja watano (5) kujishindia TZS 100,000 kila mmoja.Zawadi za Kila Mwezi: Wateja kumi (10) kujishindia TZS 200,000 kila mmoja.Siku Maalum za Cashback: Wateja watapata fedha ya kurejeshewa kulingana na thamani ya miamala yao katika tarehe zifuatazo:Black Friday – 28 Novemba 2025Cyber Monday – 1 Desemba 2025Siku ya Krismasi – 25 Desemba 2025Zawadi Kubwa Mwishoni: Washiriki watapata nafasi ya kushinda TZS milioni 5, TZS milioni 10, na zawadi kuu ya TZS milioni 15.
Akizungumzia umuhimu wa kampeni katika kuendeleza matumizi ya malipo ya kidijitali, Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali wa Benki ya Exim Silas Mtoi, alisema“Kampeni hii ni zaidi ya zawadi , inalenga kubadili namna Watanzania wanavyopata uzoefu wa malipo ya kidijitali. Tunataka wateja wajisikie urahisi, kasi na usalama wa kutumia kadi kila wanapolipa, iwe dukani au mtandaoni.
Kwa kuongeza matumizi ya kadi, tunachochea safari ya kuelekea uchumi usio na utegemezi wa fedha taslimu na kuwawezesha wateja kufanya miamala ya kidijitali na yenye usalama zaidi. Hii si kampeni ya msimu huu pekee ni hatua ya kuelekea Tanzania yenye kujiamini kidijitali.”
Wateja wanaotumia kadi za Exim pia watapata zawadi maalum wanaponunua katika maduka ya Shoppers na Village Supermarket, pamoja na punguzo maalum la msimu katika maeneo mbalimbali ya kula na burudani.
Haya ni pamoja na maeneo maarufu kama Karambezi Café, pamoja na CIP Lounge ya uwanjani, ambako wateja wa Benki ya Exim wanaweza kufurahia huduma bora zaidi wanaposafiri katika msimu huu wa sikukuu.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Banki ya Exim Stanley Kafu, alisisitiza msimamo wa benki katika kuthamini wateja: “Kampeni hii ni njia yetu ya kusherehekea na wateja msimu huu wa sikukuu.
Iwe unanunua mahitaji ya sikukuu, maandalizi ya sherehe za familia, safari za kwenda kuwatembelea wapendwa wako, kukata tiketi za mapumziko, kujaza mafuta kwa safari za barabarani, kufurahia chakula cha Krismasi na Mwaka Mpya, kununua vifaa vya sherehe, kulipia ada za shule kwa muhula ujao, au kufuatilia ofa za mtandaoni, kila ulipaji kwa kutumia kadi ya Exim unakupa urahisi, usalama, na nafasi zaidi ya kushinda msimu wote.”
Aliongeza, “Msimu huu unahusu kuleta furaha, urahisi na thamani kwa wateja wetu. Tumefanya kampeni hii kwa kusikiliza kile kinachowahusu zaidi. usalama, urahisi wa malipo na zawadi zenye maana katika kipindi hiki ambacho huwa na changamoto nyingi za kifedha.
Hii siyo promosheni tu bali ni sehemu ya ahadi yetu ya kuwathamini wateja wetu”Kafu pia alibainisha umuhimu wa kimkakati wa kampeni, akisema “Kampeni hii ni chachu muhimu katika agenda yetu ya mabadiliko ya kidijitali.
Tunataka kuwawezesha wateja kufanya malipo ya kidijitali na kufurahia faida benki yetu inayotoa.
Kadiri wateja wanavyotumia kadi dukani na mtandaoni, ndivyo tunavyosukuma mbele safari ya nchi kuelekea katika hatua ya matumizi ya fedha kidijitali, haraka na jumuishi” Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania aliipongeza Benki ya Exim kwa kuendesha kampeni inayolenga wateja wake na kutambua umuhimu wa ukweli na uwazi.
Lakini pia aliongelea mchango wa Bodi kwenye Kampeni hii: “Bodi ya Michezo inaunga mkono kikamilifu kampeni hii na itatoa usimamizi wa karibu kipindi chote cha kampeni.
Wakati wa undeshaji wa droo na kutafuta mshindi kutanedeshwa kwa kujali haki, na uwazi.
Kwa kuhakikisha kila mwenye sifa ya kushiriki anashiriki na kushinda bila kupendelewa. Wateja wanaweza kushiriki kwa kujiamini, wakijua kuwa mchakato huu ni salama na hauna upendeleo.
”Kadri matumizi ya malipo ya kidijitali yanavyozidi kukua nchini, Benki ya Exim inalenga kuongeza matumizi ya kadi, kupunguza hatari zinazohusiana na utunzaji wa fedha taslimu, na kuimarisha mfumo wa kifedha unaofanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Benki inakaribisha wateja wote kushiriki na kufurahia zawadi msimu huu.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...