Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

SERIKALI imewapatia mafunzo maalum wanahabari zaidi ya 80 ikiwa ni sehemu ya mkakati na afua muhimu ya kulifanya kundi hilo muhimu ndani ya jamii kuwa mabalozi wa kukabiliana na madhara yatokanayo na usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Wizara ya Afya, Novemba 30, 2025 yameweza kuwafumbua na kuwa na uelewa mpana kwa kundi hilo muhimu ndani ya jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam,Desemba 30,2015 wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa Taifa wa  Usugu wa Vimelea vya Magojwa Dhidi ya Dawa (UVIDA), kutoka Wizara ya Afya Bi. Emiliana Francis  amesisitiza nafasi ya wanahabari kwenye mapambano dhidi ya UVIDA.

“Elimu na ujuzi sahihi kwenu ni chachu ya kuwa mstari wa mbele kuokoa maisha, kwani mtatoa na kuandika  taarifa sahihi kwa wananchi,”amesema na kuongeza haiishii kuongeza uelewa bali pia kusaidia kupunguza vifo.

“Kwa kuwa watatumia nyenzo zao vizuri kutoa elimu kwa umma hali itakayochagiza kutumia dawa kwa usahihi na kutafuta matibabu kwa wakati.”

Kutokana na mafunzo maalum yaliyotolewa na Serikali kwa waandishi wa habari, wananchi nchini wanatarajiwa kunufaika na taarifa sahihi kuhusu matumizi ya dawa, hatua inayotarajiwa kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na UVIDA.

Kupitia mafunzo hayo, waandishi wa habari wamepatiwa mbinu za kuelimisha jamii kuhusu hatua muhimu zinazoweza kupunguza vifo vinavyotokana na usugu wa dawa, ikiwemo kutumia antibiotics pale tu zinapoandikwa na mtaalam wa afya.

Pia umuhimu wa kukamilisha dozi za dawa bila kusitisha kabla ya muda, kuepuka kujitibu bila ushauri wa kitaalam, kuchukua hatua za kinga zinazozuia maambukizi kutambua dalili hatarishi zinazohitaji matibabu ya haraka.

Kwa upande wao waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo wameahidi kutumia majukwaa yao kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka ili kuokoa maisha ya Watanzania.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...