Na Mwandishi Wetu SAME.

MKUU wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ametangaza msimamo mkali kuhusu uchimbaji wa madini ya jasi unaoendelea katika eneo la Makanya, akiagiza hatua za haraka zichukuliwe kwa kufukia mashimo yaliyotelekezwa ili kurejesha mazingira na kuimarisha usalama wa wananchi na mifugo.

Kasilda ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake katika machimbo ya madini ya viwandani (Jasi) kata ya Makanya, wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro akiambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo, ambapo alishuhudia mashimo makubwa yaliyotelekezwa pamoja na uharibifu unaofanywa karibu na barabara.

Katika ziara hiyo, Kasilda aliwaelekeza wachimbaji wa madini ya jasi pamoja na Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha mashimo yote yaliyochimbwa yanafukiwa mara moja kwani yanahatarisha usalama wa binadamu, mifugo, mazingira pamoja na miundombinu ya barabara.

“Nimeagiza mashimo yote yafukiwe mara moja ili kurejesha heshima ya mazingira na kulinda usalama wa jamii yetu, ni lazima kufuata sheria, taratibu na kanuni za uchimbaji ikiwemo kutokufanya kazi pembezoni mwa barabara na kuhakikisha kila eneo lililochimbwa linarejeshwa kama inavyotakiwa.” alisema Kasilda.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...