DIWANI wa Kata ya Butobela wilayani Geita kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paschal Mapung'o ameapa rasmi kuwatumikia wananchi wa kata hiyo katika kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani Geita.

Mapung'o aliibuka mshindi wa kiti cha udiwani kwa takribani asilimia 98 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Mapung'o ni miongoni mwa madiwani 11 wanaounda Jimbo la Busanda ambalo liko kwenye hamshauri ya Wilaya ya Geita ambapo zoezi la uapisho limefanyika Desemba 04, 2025 katika ukumbi wa halmshauri wa Wilaya ya Geita.

Kikao hicho cha uapisho kimeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Dk Alphonce Bagambabyaki ambapo jumla ya madiwani 51 wameshiriki kiapo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...