Viongozi wa kata ya Kalangalala katika halmashauri ya manispaa ya Geita leo Disemba 04, 2025 wamempokea diwani wa kata hiyo Reuben Sagayika katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wenyeviti wa mitaa ya kata hiyo, wakuu wa idara za elimu, afya na maendeleo ya Jamii na baadhi ya walimu wa shule zilizopo katika kata hiyo.

Hafla ya mapokezi imefanyika katika ofisi za kata hiyo zilizopo halmashauri ya manispaa ya Geita, akitoa taarifa ya maendeleo ya kata kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba mwaka wa fedha 2025/2026, Afisa mtendaji wa kata ya Kalangalala Bw. Emmanuel Bomani amesema wamefanikiwa kusajili wakulima 86 katika mfumo ili kuwawezesha kupata mbolea za ruzuku huku Diwani mstaafu Prudence Temba akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi Reuben Sagayika ameeleza kuwa atafanya ziara ya kutembelea mitaa yote 11 ya kata hiyo na kuzungumza na wananchi juu ya kero na masuala mbalimbali kwa maendeleo ya kata.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...