MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba ameeleza kuwa mabadiliko ya Elimu lazima yaendane na mabadiliko ya teknolojia ili kusaidia ujifunzaji na ufundishaji nchini.
Amesema hayo leo Desemba 2, 2025 Mkoani Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha uhawilishaji (Digitalisation) wa maudhui ya masomo ya Sayansi na Hisabati (STEM) kidato cha pili kwenda kwenye mfumo shirikishi wa kielektroniki utakaosaidia kuboresha Elimu kupitia ujifunzaji na ufundishaji kwa njia ya TEHAMA.
Amesema, Elimu ya Tanzania haiwezi kubaki nyuma kwenye mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayoendelea Duniani, hivyo kutoa wito kwa Wataalamu hao kuweka jitihada za kutosha ili kupata mfumo bora wenye manufaa kwa Elimu nchini.
Wakati akipita na kukagua kazi zinazoendelea kwenye majopo hayo, Dkt. Komba amewapongeza wataalamu kwa namna wanavyojitoa katika utekelezaji wa majukumu hayo, hasa kwa kuunganisha maudhui ya Elimu ya makundi ya watu wenye mahitaji maalum.
Nae, Mkuu wa Idara ya Teknolojia za Elimu Bw. Kwangu Masalu ameeleza mfumo huo utaenda kuongeza ubora wa elimu kupitia ujifunzaji na ufundishaji kwa wanafunzi wa makundi yote nchini.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...