Na Janeth Raphael MichuziTv - Dar es salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesisitiza umuhimu wa kudai haki kwa njia sahihi badala ya uharibifu, ghasia na uvunjifu wa amani walioufanya Oktoba 29, 2025, akionesha pia kusikitishwa na madai ya ugumu wa maisha unaoelezwa na baadhi yao.

Rais Samia amebainisha hayo leo Jumanne Disemba 02, 2025 wakati akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es salaam, akisema matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu yalikuwa ni matukio ya kupanga na yasiyokuwa na uhalisia.

"Ningekuwa na uwezo ningebeba Vijana wa Tanzania nikawatupa kwenye nchi tofauti Afrika na kwa majirani zetu wakaone ugumu wa maisha uliokuwepo halafu waseme kwao Tanzania ni sehemu salama. Hawana sababu. Mwenye ugumu wa maisha anahangaika kutafuta chakula chake cha leo na wengi walikuwa kwenye kazi zao."amesema Rais Samia.

"Kwanini yote yanatokea, tumejifunza kwamba Vijana wetu tumewaacha wanakua wenyewe bila muelekeo na watu wa kuwaongoza vizuri na kwa maana hiyo hawana uzalendo. 

Vijana wazalendo hata kutoka Vyama vya upinzani hawakukubaliana na hali ile na walituambia kaeni vizuri kuna hili linapangwa huku lakini Vijana wetu wengi hawana uzalendo na hilo tutakwenda kulifanyia kazi." Ameongeza kusema Rais Samia.

Rais Samia pia amewataka watafiti kufanya utafiti ndani ya Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika, na kuangalia nafasi ya Tanzania kwenye ugumu wa maisha, akisisitiza Vijana kutokubali kufuata mikumbo katika sababu zisizokuwa na uhalisia.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...