
JESHI la Polisi linapenda kujulisha kuwa, hadi jioni hii ya tarehe 10.12.2025 hali ya nchi kiusalama ni shwari na shughuli za kiuchumi na kijamii zimeendelea kufanyika katika mazingira ya amani na utulivu.
Wakati Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vikiendelea kulinda amani, usalama wa nchi, maisha ya watu na mali zao, vinapenda kuendelea kutoa wito kwa wananchi na wadau wengine endapo wanawafahamu watu waliounda na wanaoendesha makundi ya mtandaoni yenye lengo la kuandaa na kusambaza taarifa za uzushi, uchochezi, uongo na kuhamasisha vurugu vitendo ambavyo ni kinyume na sheria ya Makosa ya Kimtandao wasisite kutoa taarifa kwa siri kupitia namba zifuatazo;
0699 99 88 99, 0787 66 83 06 na kwa njia ya ujumbe kwenye mfumo kupitia kiunganishi kifuatacho https://taarifa.tpf.go.tz
Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...