Na Diana Byera,Bukoba

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera Mhandisi Johnston Mutasingwa,amewashauri waandishi wa habari wa Manispaa ya Bukoba kuibua habari za uchambuzi  zinazouhusu changamoto zinazowakabili wananchi ili zijulikane na kutafutiwa ufumbuzi wa kina.

Pia amewaomba watoe ushirikiano kwa viongozi walioko madarakani kisha kuitangaza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na serikali kwa kuandika habari za mwendelezo, ili jamii itambue miradi hiyo imefikia hatua gani na faida zake ni zipi kwasababu inatekelezwa kutokana na kodi za wananchi.

Alisema waandishi wana umuhimu mkubwa na wanaaminiwa na jamii,hivyo wanapaswa kuzingatia kuwa habari zinazotolewa zinasaidia jamii kupata taarifa sahihi na za kina kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Nyie ni wanataaluma ya habari tutumie kalamu zetu kuibua habari zenye kuvutia wasomaji na watazamaji,tuwe na mwendelezo mfano, umeandika habari inayohusu ujenzi wa soko fuatilia mpaka mwisho ili wasomaji wapende kusoma,kusikiliza na kuangalia maana,habari yenye mwendelezo inashawishi mtu aendelee kuifuatilia na hata mkandarasi ataona kama kunashinikizo atafanya vizuri "alisema Mutasingwa.

Alisema kama waandishi wa habari wataandika kwa weledi habari zao zitachangia vyombo vya habari na waandishi wake kuongeza kipato, kwasababu ikiwa ni gazeti wananchi watahakikisha wananunua magazeti ili wasome kinachoendelea,mitandaoni lazima watafungua,radio watasikiliza na Televisheni wataongeza watazamaji na wasilizaji wengi.


Aidha amewataka kutumia kalamu zao kuandika habari zenye kuchochea Amani kwasababu bila amani maendeleo hayawezi kupatikana.

Amani Kajuna ni mkazi wa mkoa wa Kagera ambaye pia alikuwa kampeni meneja wa mbunge huyo amesema waandishi wa habari ni kioo cha jamii,ni macho ya viongozi na wananchi,ni sauti ya jamii nzima ya Taifa la Tanzania hivyo, ni vyema viongozi wakashirikiana na waandishi kwani safari ya siasa inalenga maendeleo kwahiyo inahitaji ukaribu wa pamoja.

Waandishi wahabari walipata nafasi ya kuuliza maswali na kuwasilisha changamoto mbele ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba ambapo amehaidi ushirikiano kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...