Na: Calvin Gwabara – Dar es salaam.

Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) imefanya ziara ya mafunzo kwenye Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kuongeza mahusiano na kujifunza mifumo mbalimbali inayotumiwa na ofisi hiyo.

Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria Bi. Rehema Katuga (wa pili kutoka kulia) akieleza malengo ya ziara hiyo mbele ya Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo (aliyekaa katikati) na baadhi ya watumishi wengine waandamizi wa ofisi hizo mbili.

Akizungumza katika ziara hiyo, Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria Bi. Rehema Katuga amesema lengo la ziara hiyo ni kuitambulisha ofisi hiyo mpya na viongozi wake, kujifunza namna wanavyotumia mifumo mbalimbali ya kielektronic inavyofanya kazi pamoja na kudumisha ushirikiano baina ya Ofisi hizo mbili zinazotegemeana katika majukumu yao.

“Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, kama unavyofahamu ofisi yetu ni mpya imeanza rasmi mwezi wa saba mwaka huu, hivyo kuna mifumo mingi ya kiutendaji ya kielektroniki inayotumika katika utekelezaji wa majukumu na utawala ambayo na sisi tunapaswa kuwa nayo lakini tumeona ni vizuri kuja kujifunza kwenu namna inavyofanya kazi, faida zake na changamoto zake ili tunapoanza kuitumia basi tuwe na uelewa mpana ndio maana tumekuja na wataalamu wetu wote” Alisema Bi. Katuga.

Aidha ameongeza kuwa malengo ya OCPD ni kuhakikisha inaachana na matumizi makubwa ya kutumia karatasi kwenye shughuli mbalimbali za kiutendaji kwenye idara na vitengo kwa kutumia mifumo hiyo ya kielektroniki.

“Tumedhamiria kuhakikisha shughuli zote za taasisi kuanzia idara ya fedha, utawala na manunuzi na Idara za uandishi wa sheria zinatumia mifumo katika kutekeleza majukumu yake, aidha tungependa kuona mifumo hiyo inasomana ili kurahisisha utendaji wa Ofisi yetu” alifafanua Bi. Katuga.

Bi. Katuga ameishukuru Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa ushirikiano mkubwa wanaoupata katika utekelezaji wa majukumu yake na kuwasihi wasisite kuwatatafuta pale wanapokuwa na changamoto yoyote katika tafsiri ya sheria yoyote kwakuwa wao OCPD ndio wanaoziandika wanaweza kutoa ufafanuzi sahihi.

“ Kiukweli OCPD na OSG ni ofisi ambazo zinategemeana sana maana sisi OCPD tunaandika sheria zote za nchi lakini watumiaji ni nyinyi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali hivyo tupo tayari wakati wowote kuwasaidia pale mnapokumbana na Changamoto ya ufafanuzi wa sheria hizo msisite kutuona maana tunazijua vizuri zote” Alisema Bi. Katuga.

Kwa upande wake Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo amewapongeza kwa kuchagua ofisini yao kuwa mahali pazuri pa kujifunzia mifumo ya kiutendaji ya kielektroniki inavyofanya kazi na kuwaahidi ushirikiano ili waweze kupata taarifa zote wanazohitaji.

Amesema Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OSG) ni kama ndugu maana wanategemeana kwenye mambo mbalimbali ya utekelezaji wa majukumu hivyo anaamini wataweza kuendeleza ushirikiano huo katika nyanja mbalimbali za utoaji wa huduma.

“Niwahakikishie kuwa tumejipanga vizuri kwa kuwakutanisha mbele yenu na wataalamu wetu wote ambao wanashughulika na mifumo hiyo hivyo mtapata muda mzuri wa kuuliza maswali yote mnayotaka na kupata majibu yatakayosaidia kutimiza lengo la ziara yenu na tunayo mifumo mingi ambayo intumiwa na Serikali na mingine ya ndani ambayo mtaiona yote” Alisema Bi. Alice.

Ziara hiyo ya kimafunzo inajumuisha wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria ambayo ina lengo la kujifunza kwa kina namna baadhi ya Ofisi za Serikali zinavyotumia mifumo hiyo kabla ya kuanza kutengeneza mifumo yake.

MATUKO KATIKA PICHA WAKATI WA MAJADILIANO.


Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria Bi. Rehema Katuga akieleza lengo la ziara hiyo.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo akitoa neno la ukaribisho kwa menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa sheria (OCPD).

Bi. Betlanda Msolla akichangia jambo wakati wa mjadala huo hasa kuhusu mifumo ya kiutawala inavyofanyakazi kwenye ofisi hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Disheni ya Uandishi wa sheria (OCPD) Bi.Chresensia Mathayo akizungumza jambo wakati wa majadiliano na wataalamu wa ofisi ya Wakili Mkuu wa Sheri.

Bw. Francis Adolf ambaye ni Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka OCPD akichangia kwenye majadiliano hayo.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo (wa kwanza kushoto) akizungumza wkati wa majadiliano.

Bw. Alfred Nyaronga amabye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (OCPD) akifafanua kuhusu mifumo wanayolenga kijifunza kutoka OSG.

Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria wakifuatilia mawasilisho kuhusu mifumo ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inavyofanyakazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...