*Profesa Pallangyo aahidi kuendelea kuboresha miundombinu inayoendana mazingira ya sasa

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Fedha amesema kuwa wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ni hazina ya taifa kutokana na uhitaji wa usimamizi wa fedha nchini katika kuleta tija ya maendeleo ya Taifa.

imefanya mahafali yake ya 23 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiwatunuku vyeti wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu ya uhasibu wa fedha, biashara na masoko na fani nyinginezo

Naibu Waziri wa Fedha Lwesetuka aliyasema hayo katika mahafali ya 23 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam,Zanzibar pamoja na Tanga yaliyofanyika katika viwanja vya Kampasi ya Dar es Salaam.

Amesema kuwa wahitimu kazi yao kuonyesha katika kufanya kazi kwa weledi kwa kuajiriwa au kujiajiri kwa kujiletea maendeleo yao binafsi pamoja na taifa kupata maendeleo katika taaluma zao.

Amesema kuwa ujana ni kuwa wabunifu kwenye kutatua changamoto zilizopo kutokana na taaluma mlizozipata zitumike kwa maarifa , uadilifu, uwajibikaji pamoja na uzalendo wa nchi yenu Tanzania ili kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.

Alisisitiza kuwa sekta ya fedha na uhasibu ina mchango mkubwa katika kuhakikisha uwazi, ukusanyaji wa mapato na matumizi bora ya rasilimali za umma.

“Nchi inawahitaji wahasibu na wataalamu wa fedha wenye maadili, wabunifu na wanaoendana na mabadiliko ya teknolojia iwe chachu ya ajira, ubunifu na ujasiriamali,” alisema Naibu Waziri.

TIA alisema taasisi hiyo imeendelea kuboresha mitaala yake ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira na mapinduzi ya kidijitali, ikiwemo matumizi ya mifumo ya TEHAMA, uhasibu wa kisasa na usimamizi wa fedha. Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na TIA pamoja na sekta binafsi katika kuendelea kuandaa rasilimali watu yenye ushindani katika soko la ajira.

Naye Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzanua (TIA)Prof William Palangyo alibainisha kuwa mahafali ya mwaka huu yamefanyika wakati taasisi ikiendelea kupanua programu zake za kitaaluma na kuimarisha miundombinu ya kujifunzia.

Aliwashukuru wazazi na walezi kwa mchango wao katika kuwawezesha wanafunzi kufikia ndoto zao na warudi wahitimu kuwa msaada wao kuleta uhalisia wa elimu walioipata.

Profesa Palangyo mwaka wa masomo 2024/2025 chuo kimeanzisha kozi za shahada ya kwanza shahada za uzamili zinazolenga kukuza ujasirimali wa ubunifu wa usimamizi wa miradi ya maendeleo ya taifa na kuandaa wahitimu wanaoendana na uhitaji wa soko la ajira ,Teknolojia na mwelekeo wa maendeleo dira ya taifa ya 2050.

Aidha amesema kuwa Kwa mwaka 2025/2026 wanafunzi 14,209 wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.9 ikilinganishwa na wanufunzi 12263 wa mwaka wa masomo 2024/2025 na katika mwaka wa masomo 2025/2026 Serikali imegharamikia sh.bilioni 10.4 kwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania.

Katika mahafali ya 23 ya Taasisi ya uhasibu Tanzania jumla wahitimu 6334 wametunukiwa vyeti mbalimbali huku wanawake wakiwa wkiwa 3589 na wanaume wakiwa 2,245.

Katika hafla hiyo, wahitimu bora walitunukiwa tuzo maalum kwa ufaulu wa juu na nidhamu, huku wahitimu wakiahidi kuwa mabalozi wema wa taaluma zao na taasisi waliyosoma.
Naibu Waziri wa Fedha Laurent  Luswetula akizungumza katika mahafali ya 23 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)yaliyofanyika katika Viwanja vya Kampasi ya Dar es es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Profesa William Pallangyo akizungumza  maendeleo ya taasisi hiyo katika Mahafali ya 23 yaliyofanyika katika viwanja vya Kampasi ya Dar es Salaam kwa wahitimu wa Kampasi ya Dar es Salaam,Zanzibar pamoja na Tanga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) Profesa Jehovaness Aikael  akizungumza kuhusiana na ushauri wanaotoa kwa Taasisi katika kusimamia taaluma yenye ushindani  katika mahafali ya 23 ya Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Matukio mbalimbali  katika picha kwenye Mahafali  23 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA),jijini Dar es Salaam
.

Naibu Waziri wa Fedha Laurent  Luswetula akitunuku vyeti kwa wahitimu  katika mahafali ya 23 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)yaliyofanyika katika Viwanja vya Kampasi ya Dar es es Salaam.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...