Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imetoa zaidi ya shilingi milioni 800 kukamilisha ujenzi wa kituo cha Polisi ngazi ya dalaja B kilichopo Ifakara Wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro.

Akiweka jiwe la msingi katika kituo hicho kilichokamilika kwa zaidi ya asilimia 95, Mkuu wa wilaya ya Kilombero Wakili Dustan Kyoba amesema, fedha hizo zimetokana na juhudi za Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika kuhakikisha wananchi wanaishi katika hali ya usalama.

Wakaili Kyoba ametoa shukran kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa kuungana na serikali kuchangia shilingi milion 32 ili kukamilisha mifumo ya Tehama katika kituo hicho.

Dc Kyoba amesisitiza upandaji wa miti katika maeneo yanayozunguka kituo hicho, kumalizika kwa ujenzi na kuanza kazi ndani ya siku 15, kuwekeza nguvu kwenye kuzuia uhalifu wa mtandaoni maarufu halohalo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi.

Kwa upande, wake Mwakilishi wa RPC, Kamishina msaidizi wa Polisi Samuel Kijanga amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa kuhamasisha ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Ocd Kilombero, SSP David Nkuba amesema kituo hicho kimejengwa kwa forced acccount ukisimamiwa na mkandarasi wa ndani huku akihidi kukitunza.

Laison Kilwalilo, ni mkazi jirani wa eneo hilo ambaye amesema uwepo wa kituo hicho kitapelekea kupungua kwa uhalifu uliokuwa kero hapo awali.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...