Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema Tanzania imeendelea kuwa kielelezo cha amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na Duniani, akisisitiza kuwa dunia inalitazama Taifa hilo kama mfano wa kuigwa.

Guterres ameyasema Desemba 14,2025, alipokuwa akipokea ujumbe maalumu wa Tanzania uliotoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo.


Katika maelezo yake, Guterres amegusia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu akisema, ulikuwa jaribio kubwa kwa taswira ya amani ya Tanzania, lakini taifa limevuka jaribio hilo, licha ya changamoto zilizojitokeza.


“Tungependa kuona Tanzania ikiendelea kuwa taifa lililoungana na mfano bora wa amani,” amesema Guterres.


Katibu Mkuu huyo wa UN amesisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa jumuishi na yenye maana, ili kushughulikia chanzo cha matukio ya vurugu yaliyotokea wakati wa uchaguzi na kuzuia yasijirudie.


Pia ameahidi msaada wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania, hususan wakati na baada ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Serikali kukamilisha majukumu yake.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...