Na Mwandishi Wetu
VIONGOZI wa Dini wana nafasi kubwa ya kuunganisha jamii kutokana na madhara yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi.

Hayo ameyasema Mwalimu na Muumini Kanisa Katoliki Ludoovick Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema katika hatua iliyokuwepo viongozi wa dini kuendelea kuwajenga kiimani waumini katika kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote.

Amesema kuwa wakati Serikali inakwenda katika mardhiano mchango wa viongozi wa dini ni muhimu kwani wao ndio wananchi wengi wanaongoza kwenye imani ya kiroho.

Joseph amesema nafasi walionazo viongozi wa dini kama kuna changamoto wanaweza kuzitumia na sio kuwagawa wa waumini.

Mwalimu Ludovick Joseph, amesema viongozi wa dini wana haki na wajibu wa kiroho kukemea maovu yanapotokea katika jamii ili kujenga dhamiri za waumini na kutoa mwelekeo wa kimaadili kwa Taifa.

Mwalimu Ludovick amesema kauli za viongozi wa dini kuhusu masuala nyeti ya kijamii na kitaifa ni halali, kwani zina mchango mkubwa katika kuhimiza haki, amani na maadili mema miongoni mwa waumini na jamii kwa ujumla.

"Kasoro kubwa inayojitokeza ni matumizi ya lugha, akisisitiza kuwa uongeaji wa viongozi wa dini haupaswi kufanana na lugha ya wanasiasa au wapinzani wa kisiasa, bali uwe wa kidini, kichungaji na wa kimaadili," amesema.

Amefafanua kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutumia lugha ya upendo, maridhiano na hekima, huku wakiepuka kauli zinazoweza kuchochea migawanyiko au kuleta taharuki katika jamii.

Pia amekosoa wingi wa matamko kutoka kwa viongozi wa dini kwa muda mfupi, akisema si vyema kiongozi wa dini kutoa tamko leo, kesho na kesho kutwa, bali ni muhimu kutoa nafasi kwa waumini na jamii kufanya tafakari ya kina juu ya ujumbe uliotolewa.

"Nitoe wito kwa viongozi wa dini kuendelea kukemea maovu na kujenga dhamiri za waumini,

Kasoro kubwa inayojitokeza ni matumizi ya lugha, akisisitiza kuwa uongeaji wa viongozi wa dini haupaswi kufanana na lugha ya wanasiasa au wapinzani wa kisiasa, bali uwe wa kidini, kichungaji na wa kimaadili," amesema.

Amefafanua kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutumia lugha ya upendo, maridhiano na hekima, huku wakiepuka kauli zinazoweza kuchochea migawanyiko au kuleta taharuki katika jamii.

Pia amekosoa wingi wa matamko kutoka kwa viongozi wa dini kwa muda mfupi, akisema si vyema kiongozi wa dini kutoa tamko leo, kesho na kesho kutwa, bali ni muhimu kutoa nafasi kwa waumini na jamii kufanya tafakari ya kina juu ya ujumbe uliotolewa.

"Nitoe wito kwa viongozi wa dini kuendelea kukemea maovu na kujenga dhamira ya kweli kwa waumini, lakini wafanye hivyo katika mstari wa maridhiano, upendo na kusaidiana, ili kulijenga taifa lenye umoja na mshikamano kama ilivyokuwa hapo awali, "amesema Mwalimu Ludovick.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...